Home » » MAKETE WAPATIWA MAFUNZO YA ULINZI NA USALAMA WA MTOTO DHIDI YA UKATILI

MAKETE WAPATIWA MAFUNZO YA ULINZI NA USALAMA WA MTOTO DHIDI YA UKATILI

Written By kitulofm on Wednesday, 27 November 2013 | Wednesday, November 27, 2013


Na Veronica Mtauka
Mafunzo ya ulinzi na usalama wa mtoto dhidi ya ukatili na unyanyasaji yameanza kutolewa katika ukumbi wa Sumasesu kata ya Tandala wilayani Makete Mkoani Njombe kuanzia hapo jana

Mafunzo hayo yaliyofunguliwa rasmi ha;po jana na Afisa Ustawi wa jamii wilaya ya Makete Bw.Leonce Panga ambapo yamehudhuriwa na wadau mbalimbali pamoja na viongozi wa dini,dawati la jinsia kutoka kituo cha polisi Makete,maafisa elimu, magereza,mwanasheria wa halmashauri ya wilaya, ,wauguzi, pamoja na Mh.hakimu mfawidhi wa wilaya ya Makete

Katika mafunzo hayo wawezeshaji walikuwa ni Bi.Asha Mbaruku pamoja na Ramadhani Yahaya kutoka kutoka ustawi wa jamii makao makuu jijini Daresalaam ,wawezeshaji hao wamesema kuwa lengo la mafunzo hayo kwa wadau waliohudhuria ni kuwajengea uwezo washiriki namna ya kuwahudumia watoto

Washiriki hao wametakiwa kuwa timu ya ulinzi kwa na usalama kwa mtoto ili waweze kumsaidia mtoto,pia Bi.Asha amesema kuwa kuna huduma ya msaada kwa mtoto aliyefanyiwa ukatili limeanzishwa wizarani ambapo inaitwa huduma mtandao (CHILD HELPLINE) inayohusu mtoto kupiga simu moja kwa moja na kueleza shida yake na kutafutiwa suluhu

Washiriki hao pia wamefundishwa mbinu mbalimbali za ufundishaji wa masuala ya ulinzi na usalama wa mtoto kwa ngazi ya chini ya serikali

Kwa upande wao washiriki wametoa visa mbalimbali vinavyoendelea katika jamii yetu kama kata ya Mbalatse watoto wa kike kufanyiwa ukeketaji kwa siri

Mafunzo hayo pia yaliweza kuweka wazi kuhusu nini serikali imefanya dhidi ya ulinzi wa usalama wa mtoto katika masuala ya ukatili kama kutengeneza sheria ya mtoto ya mwaka 2009 kuridhia mikataba mbalimbali ya kimataifa kikanda inayohusu masuala ya ukatili dhidi ya watoto

Mafunzo hayo ya siku 5 yaliyoanza siku ya jana yameandaliwa na ustawi wa jamii makao makuu Daresalaam na yanatarajiwa kumalizika wiki hii siku ya jumamosi

Share this article :

0 comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

KITULO FM LOGO

KITULO FM LOGO
Tusikilize masaa 18 kwa siku kupitia masafa ya 97.0 FM ukiwa wilayani Makete mkoani Njombe na maeneo ya jirani

WASOMAJI WETU

KUMBUKUMBU YA HABARI ZETU

 

Copyright © 2013. KITULOFM BLOG - Haki zote zimehifadhiwa
Imetengenezwa na Edwin Moshi
Inawezeshwa na Kitulo Fm