Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe amesema ataendelea kuwa Mwenyekiti wa Chadema endapo kama wanachama wataendelea kumhitaji.
Kiongozi huyo mwenye ushawishi mkubwa
ndani ya chama chake amesema kamwe chama chake hakizuii watu kutamani
uenyekiti lakini akatahadharisha zitumike njia za kidemokrasia na
uwazi.Amesema katu Chadema hakitaruhusu watu kutumia njia za kihuni
kinyume na Katiba.
Mwenyekiti huyo ambaye ni mhimili mkuu
kwa chama chake ameshangaa watu kukimbilia madaraka kwa njia ovu na za
kihuni.Amesema kuongoza upinzani si lelemama na wala si wa
kukimbiliwa.Amesema kuongoza upinzani ni kukubali kufungwa,kupigwa
mabomu na kuzushiwa kila kashfa kila uchao.
Kiongozi huyo amesema kwamba kamwe hawatakubali Chadema kusambaratishwa kwa njia yoyote.
Kuhusu Ukomo wa uongozi amesema Katiba
ya Chadema haina kipengele hicho kwa ngazi yoyote na kama mtu anafaa
wanachama wataendelea kumchagua bila kujali muda atakaokuwa ametumikia
chama.
Source:Nipashe Jumamosi.
Home »
» MBOWE "NITAENDELEA KUIONGOZA CHADEMA WANACHAMA WAKIAMUA"
MBOWE "NITAENDELEA KUIONGOZA CHADEMA WANACHAMA WAKIAMUA"
Written By kitulofm on Monday, 25 November 2013 | Monday, November 25, 2013
Related Articles
If you enjoyed this article just click here, or subscribe to receive more great content just like it.

0 comments:
Post a Comment