Mradi
wa maji uliopo Matamba.
Kutokamilika kwa baadhi ya miradi ya maji na
mingine kujengwa chini ya kiwango kumeonekana kuwa mwiba mchungu kwa wananchi
na baadhi ya viongozi wapenda maendeleo wilayani Makete mkoani Njombe
Hayo yamebainika kwenye kikao cha kamati ya ushauri
ya wilaya (DCC) kilichofanyika katika ukumbi wa halmashauri ya wilaya ya Makete
wilayani hapa
Akizungumza kwenye kikao hicho, mwenyekiti wa
halmashauri ya wilaya ya Makete Mh. Daniel Okoka amesema kwa upande wa tarafa
ya Matamba amesema yeye kama mtia saini
mikataba ya ujenzi wa miradi hiyo hataipokea mpaka akatapofanya ukaguzi hatua
kwa hatua
"Mimi nitakwenda Matamba na kuwafuata wananchi
tunakwenda hatua kwa hatua na kuzungumza nao wakati wa ukaguzi na wakiridhika
na ujenzi huo wa mradi, mimi nitaupokea wakikataa sitaupokea" alisema
Okoka
Amesema kwa kiasi kikubwa anashangazwa na baadhi ya
viongozi wa Matamba ambao hakuwataja kumwambia kuwa hana mamlaka ya kufanya
mikutano kwenye maeneo hayo, na kufafanua kuwa yeye kama
mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Makete ana uwezo wa kufanya mikutano
sehemu yeyote ile ndani ya wilaya yake bila kizuizi, na hivyo viongozi hao
wasimkwamishe
Akichangia hoja hiyo, katibu wa CCM wilaya ya
Makete Miraji Mtaturu amesema ni aibu kwa viongozi pindi miradi ya maji
inapoonekana kutokamilika ilihali taarifa zinazotolewa zinaonesha kuwa miradi
hiyo imefanyika na imekamilika
Akizungumzia mradi wa Matamba amesema hali ni mbaya
kwani mradi huo hautoi maji licha ya taarifa kudai kuwa umekamilika, na kudai
kuwa huu si muda wa kulumbana kumtafuta mchawi na badala yake kinachotakiwa ni
maji yawafikie wananchi na si kitu kingine
Naye mwenyekiti wa kikao hicho ambaye ni Mkuu wa
wilaya ya Makete Josephine Matiro ameagiza kuwa tatizo hilo la ukosefu wa maji katika maeneo
mbalimbali yenye changamoto ikiwemo Matamba lifanywe haraka iwezekanavyo
ukizingatia kuwa serikali imetoa kipaumbele kwa miradi hiyo ya maji
0 comments:
Post a Comment