Na Veronica Mtauka
Wadau wametakiwa kujua mbinu
mbalimbali za kuwasiliana na mtoto mwenye matatizo ili waweze kuwasaidia watoto
Hayo yamesemwa na muwezeshaji
Bi.Asha Mbaruku kwenye mafunzo ya ulinzi na usalama wa mtoto kwenye ukumbi wa
sumasesu Tandala wilayani hapa mapema hii jana
Katika mafunzo hayo Bi.Asha
amesema kuwa washiriki pamoja na wadau wanatakiwa kufahamu na kutambua njia za
kuwasiliana na watoto wenye matatizo mbalimbali hasa ya ubakaji na kulawitiwa
Amesema wakati wa kuwasiliana
na mtoto wadau wanatakiwa kuangalia kauli zao ili mtoto aweze kuelezea
unyanyasaji aliofanyiwa na mtu au watu,pia wadau hao wametakiwa kufahamu ratiba
ya mtoto wakati wa mawasiliano ili kuondoa usumbufu kwa mtoto na kuzingatia
usiri wakati wa kuwasiliana nao
Aidha amesisitiza washiriki
wa mafunzo hayo pamoja na watu wa ustawi wa jamii kuangalia mambo ya kimila kwa
mtoto,suala la kidini,ulemavu,pamoja na umri wa mtoto ambaye unafanya nae
mawasiliano na wasipende kumsemea mtoto katika matatizo yake kwa mujibu wa
sheria
Mafunzo hayo ya ulinzi na
usalama wa mtoto yanaendelea huku washiriki wakifundishwa mada mbalimbali za
kupinga unyanyasaji na ukatili dhidi ya watoto ambapo mafunzo hayo yameandaliwa
na ustawi wa jamii makao makuu Dar es salaam
0 comments:
Post a Comment