Home » » VIONGOZI WAASWA KUWAJIBIKA KATIKA MAENEO YAO YA KAZI

VIONGOZI WAASWA KUWAJIBIKA KATIKA MAENEO YAO YA KAZI

Written By kitulofm on Tuesday, 19 November 2013 | Tuesday, November 19, 2013




Kufuatia kauli iliyotolewa na katibu mwenezi na itikadi wa CCM Taifa Ndugu Nape Nnauye kuhusina na baadhi ya Mawaziri kutoka chama  cha mapinduzi CCM kutowajibika kwenye nyadhifa zao na kushindwa kutatua kero za wananchi hatimaye katibu wa Chama cha Mapinduzi wilaya ya Makete Bw.Miraji Mtaturu ameunga mkono kauli hiyo na kusema suala la uwajibikaji lazima lifuatiliwe ili kuwafikishia huduma bora wananchi.
 
Katibu wa Chama cha Mapinduzi wilaya ya Makete Bw.Miraji Mtaturu
Akizungumza na kitulo fm mapema hii leo Bw.Mtaturu amesema anaunga mkono kauli hiyo na kumpongeza kiongozi huyo kwa uamuzi aliouchukua na kuhusisha uwajibikaji kwa baadhi ya viongozi wa wilaya ya Makete ambao hawawajibiki ipasavyo katika utekelezaji wa shughuli za maendeleo hususani katika mradi wa maji uliofadhiliwa na Benki ya Dunia uliopo katika tarafa ya Matamba.
 
Kifaa kinachotumika kupunguza uwingi wa maji katika eneo la kupunguzia maji
 Na Fadhili Lunati
Share this article :

0 comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

KITULO FM LOGO

KITULO FM LOGO
Tusikilize masaa 18 kwa siku kupitia masafa ya 97.0 FM ukiwa wilayani Makete mkoani Njombe na maeneo ya jirani

WASOMAJI WETU

KUMBUKUMBU YA HABARI ZETU

 

Copyright © 2013. KITULOFM BLOG - Haki zote zimehifadhiwa
Imetengenezwa na Edwin Moshi
Inawezeshwa na Kitulo Fm