MAKETE
Na:-Fadhil Lunati
Wajasiliamali wadogowadogo wilayani makete mkoani
Njombe wanaofanya biashara katika soko kuu la Iwawa wameomba kupunguziwa ushuru
kwani kipato wanachopata hakiendani na ushuru wanaotozwa nakuomba wapunguziwe
iwe sh.4000-6000 ikiwa ni pamoja na fedha ya mlinzi badala ya sh.8000
wanayolipa kwa hivi sasa.
wakizungumza na kitulo fm mapema hii leo
wajasiliamali hao wamesema ushuru wanaotozwa hauendani na kipato wanachopata
kwani hali ya usafirishaji wa bidhaa hizo ni ghali sana kutokana na miundombinu
ya barabara iliyopo kuwa mibovu kutokana na vifusi vilivyo mwagwa kutosambazwa
kwa wakati.
Aidha wajasiliamali wamezungmzia kero ya muda mrefu
ya kuvuja kwa soko hilo
kwabaadhi ya sehemu kwani walisha lalamika kwa uongozi husika lakini bado
halijatekelezwa mpaka sasa.

0 comments:
Post a Comment