Home » » WANANCHI WAONYWA JUU YA SILAHA ZA MOTO WALIZOMILIKISHWA KISHERIA

WANANCHI WAONYWA JUU YA SILAHA ZA MOTO WALIZOMILIKISHWA KISHERIA

Written By kitulofm on Thursday, 21 November 2013 | Thursday, November 21, 2013

Wananchi waonywa na jehi la polisi nchini kwa matumizi mabaya ya silaha walizomilikishwa 

Onyo hilo lilitolewa jana na Msemaji wa Jeshi la Polisi, Mrakibu Mwandamizi wa Polisi (SSP), Advera Senso, katika taarifa yake kwa vyombo vya habari na kuwataka watu hao kuacha mara moja tabia hiyo na badala yake wazingatie sheria na masharti waliyopewa wakati wa umilikishwaji.
 
Alisema kutokana na kushamiri kwa vitendo hivyo katika jamii,  jeshi hilo linaanza operesheni kali ya kuwabaini wote wanaofanya vitendo hivyo, ikiwa ni pamoja na kuwanyang’anya silaha hizo kwa wale watakaobainika kwenda kinyume cha sheria na matumizi ya silaha zao.
 
“Katika siku za hivi karibuni, imebainika baadhi ya watu waliomilikishwa silaha kihalali wamekuwa wakitumia silaha hizo kinyume cha malengo mazuri ya umilikishwaji.
 
Baadhi yao wamekuwa wakitoa vitisho kwa wananchi kwa kutumia silaha hizo bila sababu za msingi wawapo katika maeneo mbalimbali, kama vile kwenye mabaa, kumbi za starehe na hata kulipizana visasi, jambo ambalo ni kinyume cha sheria na malengo ya umilikishwaji.
 
“Jeshi la Polisi linatoa wito kwa wananchi wote wazalendo na wenye mapenzi mema na nchi yetu kutoa taarifa zitakazosaidia kuwabaini  watu wanaojihusisha na vitendo hivyo, ili waweze kukamatwa na kufikishwa kwenye vyombo vya sheria,” alisema Advera katia taarifa yake hiyo.
 
Alisema wananchi wanaweza kutoa taarifa kupitia namba ya simu 0754785557 pamoja na namba za simu za makamanda wa mikoa au kwenye kituo chochote cha Polisi.
Share this article :

0 comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

KITULO FM LOGO

KITULO FM LOGO
Tusikilize masaa 18 kwa siku kupitia masafa ya 97.0 FM ukiwa wilayani Makete mkoani Njombe na maeneo ya jirani

WASOMAJI WETU

KUMBUKUMBU YA HABARI ZETU

 

Copyright © 2013. KITULOFM BLOG - Haki zote zimehifadhiwa
Imetengenezwa na Edwin Moshi
Inawezeshwa na Kitulo Fm