Home » » MWANAMKE MMOJA AACHIWA HURU KATIKA MAHAKAMA YA (W) MAKETE

MWANAMKE MMOJA AACHIWA HURU KATIKA MAHAKAMA YA (W) MAKETE

Written By kitulofm on Friday, 6 December 2013 | Friday, December 06, 2013

Mahakama ya wilaya ya makete imemuachia huru Bi.Agness Tweve mkazi wa kijiji cha Iwawa kata ya Iwawa wilayani Makete Mkoani Njombe alikuwa anatuhumiwa kwa kosa la kumjeruhi Donad Daud Sanga mkazi wa Iwawa Wilayani hapa.


Akitoa hukumu ya kumuachia huru bila masharti Hakimu wa Mahakama ya wilaya ya Makete Mh.John Kapokolo amesema kuwa Mahakama inamuachia huru mtuhumiwa kutokana na ushahidi uliotolewa kutokuwa na vielelezo vya kuaminika mahakamani kuwa mtuhumiwa huyo alitenda kosa hilo.

Hata hivyo ushahidi uliotolewa haukuwa wawazi na kubainisha namna gani mjeruhiwa ajeruhiwa na kuathirika kwa kiasi gani kwani inaonyesha mshitakiwa alipatwa na hali mbaya      

Wakati huo huo ndugu Manenge Sanga mwenye umri wamiaka 40 mkazi wa Ilevelo kata ya Lupalilo wilayani Makete anatuhumiwa kwa kosa la kumbaka mwanamke mmoja (jina limehifadhiwa)mwenye umri wa miaka 65 mkazi wa kijiji cha Ilevelo.

Akisoma mashtaka hayo mwendesha mashtaka wa jeshi la Polisi Wilayani Makete Bw.Gozbet Millikion Komba amesema mtuhumiwa alitenda kosa hilo mnamo tarehe 7 Julai 2013 saa mbili usiku katika kijiji cha ilevelo ambapo alimvamia mshtaki akiwa nyumbani kwake na kumbaka  mama huyo ambae pia ni Mjane .

Hata hivyo mshitakiwa amekana kuhusika na mashitaka,ikiwa mwendesha mashitaka wa polisi Bw.Komba ameiomba Mahakama kuwaleta mashahidi wa shitaka hilo katika tarehe iliyopangwa tarehe 20 Desemba mwaka huu.
 Na Henrick Idawa
Share this article :

0 comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

KITULO FM LOGO

KITULO FM LOGO
Tusikilize masaa 18 kwa siku kupitia masafa ya 97.0 FM ukiwa wilayani Makete mkoani Njombe na maeneo ya jirani

WASOMAJI WETU

KUMBUKUMBU YA HABARI ZETU

 

Copyright © 2013. KITULOFM BLOG - Haki zote zimehifadhiwa
Imetengenezwa na Edwin Moshi
Inawezeshwa na Kitulo Fm