Na Furahisha Nundu
Akitoa elimu hiyo kwa
wanafunzi wa chuo cha St.Augustine Mkuu wa TAKUKURU wilaya ya Makete Bw.Daudi
Joshua ameelezea njia za kuzuia na kupambana na rushwa ikiwa rushwa ni Chanzo
cha kushuka kwa maadili na kusababisha kuporomoka kwa uchumi katika Taifa zima
Amesema kuwa wanafunzi katika
ngazi tofauti wamekuwa wakikumbana na rushwa aina mbalimbali ikiwemo ya ngono
ili kupata jambo Fulani kitu ambacho ni hatari katika taasisi ya TAKUKURU hivyo
wawe makini katika kusababisha na kuzuia rushwa
Zaidi ya wanafunzi 16
wamepatiwa mafunzo hayo ikiwa kwa upande wa wanafunzi wenyewe wameshukuru kwa
Taasisi hiyo kwa kutoa elimu hiyo ambapo taasisi hiyo ilianza mwaka 2007 kuunda vilabu vya kuzuia na kupambana na Rushwa katika shule za Sekondari wilayani hapa hata hivyo taasisi hiyo
inampango wa kuunda vilabu katika shule za msingi zilizopo wilayani Makete
0 comments:
Post a Comment