Kutokana na wananchi wa wilaya ya Makete kulalamikia upandaji wa bei ya kilo moja ya ya nyama ya Ng'ombe kupanda kutoka sh 5,000/= hadi shilingi 6,000/=, suala hilo limeibua mjadala mzito kwenye baraza la madiwani wa halmashauri ya wilaya ya Makete kwa madai kuwa upandaji huo wa bei umekiuka maamuzi halali ya vikao vilivyoazimia bei iwe sh. 5000/=
Akitoa taarifa kwenye baraza hilo la madiwani Afisa biashara wilaya ya Makete Bw. Edonia mahenge amesema ni kweli wamefanya kikao na kuazimia kupandisha bei ya nyama ya ng'ombe ambapo kwa hivi sasa itakuwa ikiuzwa kwa bei ya tsh. 6000/- kwa kilo moja
Amesema sababu za kupandisha bei ni kutokana na kupanda kwa gharama za uendeshaji wa biashara hiyo ikiwemo, kupanda kwa bei ya ng'ombe, kupanda kwa ushuru wanaolipa kwa halmashauri pamoja na gharama nyingine ambazo zimepanda kwa muda mrefu lakini bei ya nyama inazidi kubaki vile vile
Bw. Mahenge amesema wamefanya mawasiliano na maeneo mbalimbali ndani ya mkoa wa Njombe ikiwemo makambako ambapo wamegundua kuwa bei ya nyama kwa maeneo hayo imepanda kutoka sh. 5,000/= na kufikia 6,000/=
Maelezo hayo yalionesha kuwachefua baadhi ya madiwani ambao wamesema Afisa biashara huyo amekiuka utaratibu wa vikao vya maamuzi vilivyoazimia kuwa nyama iuzwe sh. 5000/= kwa kilo na alitakiwa kuja kutaarifu vikao kuwa wanataka kupandisha bei ya nyama na si kuipandisha kwa kushtukiza
Hata hivyo Diwani wa kata ya Bulongwa mh. Erica Sanga amesema biashara hii ni huria hivyo haina haja ya kuendelea kuijadili na badala yake wasimamie bei ambayo haiwezi kuwaumiza wananchi ambapo kama gharama mbalimbali zimepanda ikiwemo ushuru wanaolipa kwa halmashauri basi bei hiyo ni lazima ipande
Hata hivyo Mkuu wa wilaya ya Makete Mh Josephine Matiro ametolea ufafanuzi katika baraza hilo na kusema kuwa kama wafanyabiashara hao wa nyama wamekuwa wakipandishiwa gharama kila mwaka ilihali bei ya nyama haipandi, huko ni kuwaumiza na kutowatendea haki wafanyabiashara hao
Mh. Matiro amesema kama halmashauri imeshawapandishia ushuru ni dhahiri kuwa na bei ya nyama itapanda hivyo bei hiyo ya sh. 6,000/= imepanda kutokana na gharama zilizopanda kwenye biashara hiyo wanayoifanya
Wiki iliyopita halmashauri ya wilaya ya makete kupitia kwa Afisa biashara wake Bw. Edonia Mahenge walitangaza kipanda kwa bei ya nyama kutoka 5,000/= hadi 6,000/= kwa kilo moja hali iliyolalamikiwa na wananchi kuwa bei hiyo inawaumiza
Baraza hilo limeafiki bei ya nyama iuzwe sh. 6,000/= kutokana na sababu zilizoainishwa na afisa biashara

Na Edwin Moshi

0 comments:
Post a Comment