Mbunge wa wilaya ya Makete Mh.Binilith Mahenge ameendelea na zoezi la
ugawaji wa vitabu ktk shule za Sekondari zilizopo Wilani Makete ambapo leo hii
amegawa zaidi a vitabu mia mbili ktk shule ya sekondali Bulongwa
Akikabidhi vitabu hivyo kwa mkuu wa shule hiyo Aksoni Ntulo mbele ya
wananchi Mahenge amewasihi wazazi na walezi wa watoto kuwapeleka wanafunzi
waliochaguliwa kuiunga na masomo ya sekondari kaika shule walizochaguliwa.
Kwa upande wake Mkuu wa shule ya sekondari Bulongwa Mwl.Aksoni Ntulo
amemshukuru Mh.Mbunge kwa msaada wa vitabu hivyo kwani hivi sasa anauhakika shule yake itaongeza ufaulu kwa wanafunzi kulingana na vifaa vya shule kuongezeka hivyo kila mwanafunzi atakuwa na uhakika wa ksoma kwa raha bila kung'ang'aniana vitabu pindi wawapo Darasani
Hata hivyo Penye nia pana njia japo kila penye mafanikio hazikosi changamoto kwani shule hiyo inakabiliwa na changamoto kubwa ya upungufu wa vifaa vya maabara.
0 comments:
Post a Comment