Makamu
mwenyekiti taifa wa chama cha mapinduzi (CCM) Phillip Mangula amewataka
viongozi wa matawi kusimamia ipasavyo kanuni za uchaguzi na uongozi na
maadili wa chama hicho kwa kupiga vita rushwa hasa kuelekea katika
chaguzi za serikali za mitaa zinatarajiwa kufanyika mwaka huu.
Kauli
hiyo ameitoa leo jijini Dar es salaam katika salama za mwaka wakati
akizungumza na wajumbe wa halmashauri kuu ya tawi la ofisi ndogo za
chama hicho lilipo Mtaa wa Lumumba.
Amewataka
viongozi hao kuweka misingi mizuri ambayo itawezesha kupatikana
viongozi wazuri ambao hawatokani na mianya ya rushwa ili kuwa na dira
nzuri kuelekea katika uchaguzi Mkuu utakaofanyika 2015.
“Nataka
kanuni za uchaguzi na uongozi na maadili ziheshimiwe ili kupata
viongozi ambao hawatatokana na rushwa, na hakikisheni katika vikao vyenu
vya chama mnasimamia agenda mbili ambayo ni uchaguzi na kujadili
mwenendo wa katiba mpya”
“Mkifualia
hatua moja hadi nyingine katika mchakato wa kuipata katiba kuanzia
ushiriki wa wajumbe wa bunge maalum hadi katika mjadala wa wajumbe
wakipitia kifungu kimoja hadi kingine mtakuwa na nafasi kubwa ya kutoa
maoni yenu pale itakaporudi kwa wananchi,”alisema Mangulla.
Akizungumzia
uwepo wa serikali tatu katika rasimu ya katiba mpya, Mangula amesema
bado ni mapema mno kuzungumzia hatia ya suala hilo kwani mchakato wa
kuipata katiba bado mrefu ambao mbali na wawakilishi wa bunge maalumu la
katiba utashirikisha tena wananchi ambao watapiga kura yao ya mwisho.
Mbali
na kuwapongeza tume ya katiba mpya kwa kufanya kazi kwa uwazi,
amewapongeza wanachama wa ccm kwa jinsi walivyoshirikia ama mmoja mmoja
au katika kundi katika kuhakikisha wanatoa maoni yao katika rasimu ya
katiba ambayo imewasilishwa kwa Rais Jakaya Kikwete mwishoni mwa mwaka
jana.

0 comments:
Post a Comment