Home » » WANYAMA AINA YA NYANI WASHAMBULIA MAZAO MAKETE

WANYAMA AINA YA NYANI WASHAMBULIA MAZAO MAKETE

Written By kitulofm on Monday, 6 January 2014 | Monday, January 06, 2014



Wakulima wa viazi wanaolima eneo la ujamaa katika kijiji cha Mbanga wilayani makete wanapata hofu ya kutopata mazao mazuri baada ya nyani kuvamia mashamba yao

Wakizungumza na kitulo fm kwa nyakati tofauti wakulima hao wamesema wanapata shida  sana kwani wanyama hao aina ya nyani wamekuwa waharibifu sana kwenye mazao yao

Wakulim hao mara nyingi hujitahidi kulinda mazao yao kwa kutumia mbwa  na wakati mwingine hulazimika kutumia njia mbadala ya kuwafunga mbwa katika mashamba yao ili kunusuru hali ya mazao yao

Pia wameongeza kuwa wakulima wengi wa eneo hilo hutegemea sana kilimo cha mazao ya viazi,ngano na mahindi lakini pindi mazao hayo yanapofikia hatua ya kukomaa nyani hao hushambulia mazao hayo na kuongeza kuwa huwa wanapata shida sana namna ya kuwadhibiti kwani shughuli zao za kilimo zipo karibu na misitu ambapo misitu ndio makazi ya nyani hao


Share this article :

0 comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

KITULO FM LOGO

KITULO FM LOGO
Tusikilize masaa 18 kwa siku kupitia masafa ya 97.0 FM ukiwa wilayani Makete mkoani Njombe na maeneo ya jirani

WASOMAJI WETU

KUMBUKUMBU YA HABARI ZETU

 

Copyright © 2013. KITULOFM BLOG - Haki zote zimehifadhiwa
Imetengenezwa na Edwin Moshi
Inawezeshwa na Kitulo Fm