Home » » BWENI LA NJOMBE SEC SCHOOL LILILOUNGUA LAINGIZA HASARA YA ZAIDI MILIONI 63

BWENI LA NJOMBE SEC SCHOOL LILILOUNGUA LAINGIZA HASARA YA ZAIDI MILIONI 63

Written By kitulofm on Tuesday, 4 February 2014 | Tuesday, February 04, 2014

Jeshi la Polisi Mkoani Njombe Linawashikilia Watu Watatu Kwa Tuhuma za Mauaji ya Bi Getrude Kaduma Mkazi wa Kijiji Cha Ihawanga Wilaya ya Mufindi Mkoani Iringa.

Kamanda wa Polisi Mkoani Njombe Fulgency Ngonyani Amewataja Watu Hao Wanaoshikiliwa Kuwa ni Japhari Malekela Mkazi wa Kijiji Cha Ihawanga,Alatumisa Shigola Mkazi wa Ihawanga na Felishina Kaduma Mkazi wa Kijiji Cha Nyamande.

Akizungumzia Tukio Hilo Kamanda Ngonyani Amesema Kuwa Mnamo Feb Mbili Mwaka Huu Majira ya Saa Mbili Usiku Katika Kijiji Cha Nyamande Kata ya Kitandililo,Tarafa ya Makambako Mkoani Njombe Watuhumiwa Walimbaka Marehemu na Kisha Kumuua.

Amesema Kabla ya Kuuawa Marehemu Alibakwa na Kisha Kunyongwa Shingo na Watu Hao Ambao Jeshi la Polisi Pamoja na Kuwashikilia Watuhumiwa Hao Bado Linaendelea na 
Uchunguzi Ili Kubaini Chanz0 Cha Tukio Hilo.

Katika Tukio Jingine Mkazi wa Kijiji Cha Uhenga Kata ya Saja Wilayani Wanging'ombe Mkoani Njombe Waidu Lupenza Amefariki Dunia Baada ya Kujinyonga Ikiwa ni Katika Kile Kinachodaiwa Kuwa ni Kutokana na Kusumbuliwa na Ugonjwa wa Malaria Pamoja na Maumizi Makali ya Kichwa.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Njombe Fulgency Ngonyani Amesema Tukio Hilo Limetokea Feb Mosi Mwaka Huu Majira ya Saa Kumi na Mbili Jioni Katika Kijiji Hicho Baada ya Mke wa Marehemu Kwenda Dukani Kutaufta na Ndipo Aliporudi Nyumbani na Kumkuta Mumewe Akiwa Tayari Amefariki Kwa Kujinyonga

Amesema Mwili wa Marehemu Ulikutwa Ukining'inia Juu ya Kenchi la Nyumba Hiyo Baada ya Marehemu Kujinyonga Kwa Kutumia Upande wa Kanga na Hivyo Kwa Kuwa Marehemu Hakuacha Ujumbe Hivyo Jeshi la Polisi Linaendelea na Uchunguzi Ili Kubaini Chanzo Cha Tukio Hilo.

Wakati Huo Huo Mkazi Mmoja wa Mji Mwema Mjini Njombe Ambae Jina Lake Halikuweza Kufahamika Mara Moja Amefariki Dunia Baada ya Kugongwa na Gari Katika Barabara Kuu ya Njombe-Songea Eneo la Mji Mwema Mjini Njombe.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Njombe Fulgency Ngonyani Amethibitisha Kutokea Kwa Tukio Hilo na Kusema Kuwa Jeshi Hilo Kwasasa Linamshikilia Aloyce Mtege Mmiliki na Dereva wa Gari Hilo Kwa  Mahojiano Zaidi Kutokana na Tukio Hilo.

Kufuatia Matukio Hayo Jeshi la Polisi Mkoani Hapa Linakiri Kuwa Matukio ya Mauaji na Watu Kupoteza Maisha Katika Mazingira Tofauti Imeendelea Kuwa Changamoto Kubwa Kwa Jeshi Hilo.

Katika Hatua Nyingine Jeshi la Polisi Mkoani Njombe Limethibitisha Kutokea Kwa Wizi wa Pikipiki Katika Kijiji Cha Lusitu Wilayani Njombe Baada ya Watu Wasiofahamika Kuiba Pikipiki Aina ya T-Better Yenye Thamani ya Zaidi ya Shillingi Millioni Moja Mali ya Pilimin Mlowe Mkazi wa Kijiji Cha Lusitu.

Aidha Jeshi la Polisi Mkoani Njombe Limethibitisha Juu ya Chanzo Cha Ajali ya Moto Iliotokea Katika Shule ya Secondary Njombe na Kusababisha Hasara Kwa Wanafunzi wa Shule Hiyo.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Njombe Fulgency Ngonyani Amesema Chanzo Cha Ajali Hiyo ni Kutokana na Hitilafu ya Umeme Iliotokea Kwenye Bweni Hilo la Wavulana Mchanganyiko wa Kidato Cha Tano na Cha Sita Takribani 42 Waliokuwa Wakitumia Bweni Hilo.

Amesema Miongoni Mwa Mali Zilizoharibika Kutokana na Ajali Hiyo ni Pamoja na Vitanda,Magodoro,Mabegi ya Nguo,Masanduku ya Vitabu Ambavyo ni Mali za Wanafunzi 42 Waliokuwa Wakitumia Bweni Hilo.

Ameongeza Kuwa Hadi Sasa Hakuna Madhara Yoyote Yaliotokea Kwa Binadamu na Hivyo Jeshi la Polisi Bado Linaendelea na Uchunguzi wa Tukio Hilo na Hadi Sasa Thamani ya Mali Zote Zilizoungua Pamoja na Jengo Hilo Bado Haijafahamika.

Akizungumzia Tukio Hilo Diwani wa Kata ya Mji Mwema Mkoani Njombe Jimmy Ngumbuke Amesema Kwa Mujibu Taarifa Zilizotolewa na Uongozi wa Shule Hiyo Hasara Iliotokana na Ajali Hiyo Inakadiriwa Kufikia Zaidi ya Shilling Millioni Sitini na Tatu
Share this article :

0 comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

KITULO FM LOGO

KITULO FM LOGO
Tusikilize masaa 18 kwa siku kupitia masafa ya 97.0 FM ukiwa wilayani Makete mkoani Njombe na maeneo ya jirani

WASOMAJI WETU

KUMBUKUMBU YA HABARI ZETU

 

Copyright © 2013. KITULOFM BLOG - Haki zote zimehifadhiwa
Imetengenezwa na Edwin Moshi
Inawezeshwa na Kitulo Fm