Picha na Edwin Moshi
Sifa ya mbaya ya wilaya ya Makete Mkoani Njombe kuwa na idadi kubwa ya maambukizi ya virusi vya Ukimwi kwa miaka mingi sasa imeanza kuwa sifa nzuri baada ya Mkuu wa Mkoa wa Njombe Kapten Asseri Msangi kuuleza umma wa wanamakete kuwa idadi ya maambukizi ya virusi vya Ukimwi wilayani Makete inaendelea kupungua mwaka hadi mwaka

Sifa
nzuri ya kuashiria kwamba wanamakete hivi sasa wameelimika kuhusu maambukizi ya
virusi vya Ukimwi inazidi kupungua imeonekana kuwafurahisha wanamakete kwani
wengi wao walikuwa na wasiwasi kila wanapokuwa wanafikiri kuhusu gonjwa hili
Hatari la Ukimwi kwani limesababisha watoto wengi kuishi mazingira ya watoto
yatima na Magumu
Kauli
hiyo ilizungumzwa na Mkuu wa Mkoa wa Njombe Asseri Msangi katika maadhimisho ya
siku ya Maji Duniani ambapo mkoani Njombe maadhimisho hayo yalifanyika katika
Wilaya ya Makete katika viwanja vya Mabehewani Makete Mjini mnamo tarehe 22
March 2014
Hata
hivyo Msangi amesema kuwa mpaka sasa bado wilaya ya Makete imeendelea kukumbwa
na changamoto kubwa ya kuwa na watoto yatima
wengi ambao wazazi wao kwa kiasi kikubwa walikufa kwa maambukizi ya
virusi vya Ukimwi Ukimwi
Hivyo
Kitulofm blog na Kitulo fm Redio inatoa rai kwa wanamakete kuishi kwa tahadhari
juu ya maambukizi ya Virusi vya Ukimwi wasibweteke na sifa nzuri ambayo
wameanza kuipata sasa badala yake wakawa makini ili kutokomeza kabisa gonjwa
hili hatari la Ukimwi
Na Furahisha Nundu
0 comments:
Post a Comment