Na Edwin Moshi
Mbunge
Lekule Laiza amemuomba mwenyekiti wa bunge maalum la katiba Mh. Samwel
Sitta kumwandikia barua Rais Dkt Jakaya Kikwete barua ya kulivunja bunge
hilo kwa kuwa wameshindwa kazi
Mh.
Laiza ametoa kauli hiyo leo Machi 27, bungeni wakati akichangia hoja
kuhusu upigaji wa kura ya siri ama upigaji wa kura ya wazi, na kusema
kuwa wananchi wamekuwa wakiwapigia simu na kuwataka warudi majumbani kwa
kuwa wameshindwa kazi
"Kama
kazi imetushinda na tunashindwa kufikia muafaka, ni heri mwenyekiti
umwandikie rais barua avunje bunge hili, turudi majumbani" amesema Laiza
Amesema
kuwa kutokana na bunge hilo kughubikwa na vihoja vya mara kwa mara ni
dhahiri kuwa suala hilo limekuwa likiwaumiza vichwa lakini kutokana na
umuhimu wa katiba yeye ameshindwa kuona kuwa wao kama wabunge wanafanya
nini bungeni, hivyo wanatakiwa kuondoka na kurudi kwao kwa kuwa kazi
imewashinda
Kauli
hiyo imepingwa vikali na mbunge wa Arumeru mashariki Mh. Joshua
Nassari wakati akichangia hoja na kusema kuwa kwa kuwa wamekuja kwa
ajili ya katiba, anataka bunge hilo liendelee mpaka kieleweke
kilichowaleta yaani kupata katiba mpya kwa kuwa kodi za watanzania
zinaendelea kutumika na hivyo inatakiwa waendelee
"nimetoka
jimboni kwangu jana tu na ndiyo maana nimeapishwa leo, wananchi
wanataka kura ya siri na pia wanataka katiba mpya" alisema Nasari
0 comments:
Post a Comment