Mkuu
wa Mkoa wa Njombe Captain Mstaafu Asseri Msangi Amevitaka Vyombo Vya Habari
Mkoani Hapa Kufanya Kazi Kubwa ya Kuendelea Kuibua na Kuandika Mambo Mbalimbali
Yaliyojificha Ili Kuisaidia Jamii Kuondoka na Matatizo Yasiyo Ya Lazima.
Capteni Mstaafu Asseri Msangi Ameyasema Hayo Alipo Kuwa Mgeni Rasmi
Katika Maadhimiosho ya Miaka Minne Tangu Kuanzishwa Kwa Kampuni Ya Daraja Letu
Katika Mikoa ya Njombe na Iringa.
Capteni Msangi Amesema Kuwa Kutokana na Kuwepo Kwa Changamoto Nyingi Zilizopo Katika Jamii na Kisha Kushindwa Kuifikia Serikali Kwa Wakati Ni Vyema Vyombo vya habari vikafanya Kazi Ya Ziada Katika Kuhakikisha Serikali Inayapata Matatizo na Changamoto Hizo Ili Ziweze Kupatiwa Ufumbuzi.
Capteni Msangi Amesema Kuwa Kutokana na Kuwepo Kwa Changamoto Nyingi Zilizopo Katika Jamii na Kisha Kushindwa Kuifikia Serikali Kwa Wakati Ni Vyema Vyombo vya habari vikafanya Kazi Ya Ziada Katika Kuhakikisha Serikali Inayapata Matatizo na Changamoto Hizo Ili Ziweze Kupatiwa Ufumbuzi.
Pamoja na Mambo Mengine Msangi Amevitaka vyombo vya habari Kuendelea Kuwaandika na kutoa taarifa zinazohusu Viongozi Wabadhilifu,Wanaoshindwa Kutekeleza Majukumu Yao Kwani Kwa Kufanya Hivyo Kutawafanya Kuzingatia Maadili ya Utumishi wa Umma.
Sanjari na Hilo Lakini Pia Amesema Mkoa wa Njombe Umekuwa Ukikabiliwa na Changamoto Mbalimbali Ambazo Bila Vyombo Vya Habari Haziwezi Kutatuliwa Huku Akiwataka Wanahabari Kufanya Kazi Zao Kwa Weledi na Kwa Kuzingatia Maadili Ya Uandishi wa Habari Ili Kuepusha Mgongano Baina Ya Viongozi Husika na Wananchi Wanao Waongoza.
Josephine Sebastian Lemoyan ni Mjumbe wa Bodi Ya Kampuni ya Daraja Letu Ambaye Amesema Daraja Letu ni Shirika Linalojishughulisha na Mambo Mbalimbali Ikiwemo Kuibua Miradi Ya Kimaendeleo Katika Jamii Pamoja na Kuitekeleza.
Aidha Bi.Lemoyan Amesema Kuwa Daraja Kupitia Gazeti Lake Limekuwa Likifanya Kazi Kubwa Ambapo Hadi Sasa Limekuwa Likifanya Tafiti Ndogondogo Zinazoendana na Wakati,Kuibua Mambo Yaliyojificha Zikiwemo Changamoto za Sekta ya Elimu,Afya,Miundombinu Pamoja na Huduma za Maji Ambazo Baadhi Zimeweza Kupatiwa Ufumbuzi
0 comments:
Post a Comment