Home » » WAJASIRIAMALI MAKETE NJOMBE WAPATA MAFUNZO KUTOKA TRA

WAJASIRIAMALI MAKETE NJOMBE WAPATA MAFUNZO KUTOKA TRA

Written By kitulofm on Wednesday, 19 March 2014 | Wednesday, March 19, 2014

Jamii wilayani Makete Mkoa wa Njombe imeelezwa juu ya umuhimu wa elimu ya ujasiriamali ili kuwa na biashara endelevu kwa kuongeza pato la Familia na Taifa kwa ujumla
Kaimu Meneja wa TRA Wilaya ya Makete Aron Zumba akitoa maelezo katika Semiana hiyo kwa wajasiriamali
Hayo yameelezwa na Meneja wa Mamlaka na Mapato Tanzania TRA huduma na elimu Mkoa wa Iringa na Nombe Bw.Gerald Hill mapema hii leo kwa wafanyabiashara wakubwa na wadogo wilayani hapa katika semina inayohusu inayohusu wajasiriamali wadogo na wakubwa iiyofanyika katika ukumbi wa kata Iwawa Makete Mjini
Meneja wa Mamlaka ya Mapato Tanzania(TRA)huduma na mapato mkoa wa Iringa na Njombe Gabrie Hill

Bw.Gerald amesema kuwa ni muhimu wajasiriamali kupata elimu inayohusu wajasiriamali lengo likiwa ni mjasiriamali aweze kuendelea na kukuza biashara yake,Kujenga uhusiano mzuri kati ya Mamlaka ya Mapato Tanzania TRA na walipa Kodi

Nao wajasiririamali waliokuwepo katika semina hiyo wameiomba TRA kuwapunguzia Gharama za kodi ambapo wameongeza kuwa zoezi la bomoa bomoa lililofanyika mwishoni mwa mwaka jana kubomoa vibanda eneo la Makete mjini limewaathiri kwa kiasi kikubwa


Zaidi ya wajasiriamali 50 kutoka katika Kata ya Iwawa Makete mjini wameweza kufika katika semina na kunufaika na Mafunzo hayo pamoja na kutoa kero zao kuhusu malipo ya kodi kuwa juu

Na Furahisha Nundu
Share this article :

0 comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

KITULO FM LOGO

KITULO FM LOGO
Tusikilize masaa 18 kwa siku kupitia masafa ya 97.0 FM ukiwa wilayani Makete mkoani Njombe na maeneo ya jirani

WASOMAJI WETU

KUMBUKUMBU YA HABARI ZETU

 

Copyright © 2013. KITULOFM BLOG - Haki zote zimehifadhiwa
Imetengenezwa na Edwin Moshi
Inawezeshwa na Kitulo Fm