Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akisikiliza maelezo kuhusu Chungu na Vibuyu, vilivyotumika kuchanganya
Udongo wa Tanganyika na Zanzibar, mwaka 1964, kutoka kwa Mawazo Ramadhan
wa Makumbusho ya Taifa, wakati alipotembelea kwenye Banda la Idara ya
Muungano Ofisi ya Makamu wa Rais, alipotembelea maonyesho ya Sherehe za
maadhimisho ya miaka 50 ya Muungano yanayoendelea kwenye Viwanja vya
Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam. (Picha na OMR).
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akionyeshwa na Ofisa wa Idara ya Muungano Ofisi ya Makamu wa Rais,
Martha Mashuki, baadhi ya Magazeti yaliyochapishwa mwaka 1964, wakati
alipotembelea kwenye Banda la Idara ya Muungano Ofisi ya Makamu wa Rais,
alipotembelea maonyesho ya Sherehe za maadhimisho ya miaka 50 ya
Muungano yanayoendelea kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es
Salaam.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akipata maelezo kuhusu shughuli za Bunge kutoka kwa Ofisa Habari wa
Bunge, Prosper Minja, wakati alipotembelea kwenye Banda hilo, kwenye
maonyesho ya Sherehe za maadhimisho ya miaka 50 ya Muungano
yanayoendelea kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
apata maelezo kutoka kwa Naibu Katibu Mtendaji wa TCU, Prof. Magishi
Mgasa, alipokuwa akitembelea kwenye Mabanda ya maonyesho ya Sherehe za
maadhimisho ya miaka 50 ya Muungano yanayoendelea kwenye Viwanja vya
Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam. (Picha na OMR).
0 comments:
Post a Comment