Waziri wa Mali asili na Utaliii na Mbunge wa jimbo la Singida kaskazini,Lazaro Nyalandu.
Na Nathaniel Limu, Singida
KANISA
jipya la Miracle Assemblies of God Ministry (MAGM) mkoani Singida
linatarajia kutumia zaidi ya shilingi 214.1 milioni kugharamia ujenzi wa
shule ya awali ya bweni.
Hayo
yalisemwa hivi karibuni na Magreth Ndwete wakati akisoma risala fupi ya
kanisa hilo kwenye hafla ya kusimikwa kwa askofu wa kwanza wa kanisa
hilo John Sanongo Tesha (58), Mgeni rasmi katika hafla hiyo,alikuwa
Waziri wa Mali asili na Utaliii na Mbunge wa jimbo la Singida
kaskazini,Lazaro Nyalandu.
Amesema
shule hiyo ambayo tayari imeisha anza kwa kuwa na vyumba viwili vya
madarasa itachukua wanafunzi wa madhehebu yote ya dini na wale ambao
hawana dini kama watakuwepo.
Amesema
kanisa hilo lililoanza rasmi juni 11 mwaka 2007 na kupata usajili
novemba 21 mwaka jana,pamoja na kutoa huduma ya kiroho pia limeamua
kutoa huduma ya kijamii kwa kuanzisha shule ya awali.
“Kwa
kuanzia waumini wa kanisa hilo waliamua kuchangishana wao kwa wao na
kufanikiwa kupata zaidi ya shilingi 17.8 milioni ambazo zimegharamia
ujenzi wa vyumba viwili vya madarasa ambavyo hivi sasa
vinatumika”amesema Ndwete.
Aidha,
amesema kwa kuanzia wanatarajia kuanza na wanafunzi 80 na lengo ni
kuongeza wanafunzi kadri Mungu atakavyowawezesha kuwa na uwezo wa
kuongeza vyumba vya madarasa na mabweni.
“Uongozi
wa kanisa la Miracle unatoa shukrani kwa waumini wake wote waliojitolea
kwa hali na mali,kuhakikisha kuwa kanisa hilo limefikia hatu hii nzuri
tunayoiona”,amesema.
Wakati
huo huo,mgeni rasmi Waziri Nyalandu ameahidi kulichangia kanisa hilo
zaidi ya shilingi 75 milioni,ili liweze kupiga hatua katika ustawi wake.
CHANZO:MO-BLOG
0 comments:
Post a Comment