Home » » MH.HALIMA MDEE ATUNUKIWA TUZO YA MWANASIASA BORA ZAIDI WA KIKE BARANI AFRIKA

MH.HALIMA MDEE ATUNUKIWA TUZO YA MWANASIASA BORA ZAIDI WA KIKE BARANI AFRIKA

Written By kitulofm on Wednesday, 9 April 2014 | Wednesday, April 09, 2014

Mbunge wa Kawe (Chadema) Halima Mdee na Mkurugenzi wa Jukwaa la Uchumi la Dunia kwa Bara la Afrika(WEF) Elsie Kanza, ni miongoni mwa viongozi wanawake 11 wa kisiasa kutoka barani Afrika waliotunukiwa tuzo ya kuwa viogozi wanawake wa juu wenye nguvu katika siasa.

Mdee ambaye pia ni Waziri kivuli wa Wizara ya Ardhi, nyumba na Maendeleo ya Makazi, aliunganishwa katika orodha ya wanawake jasiri katika masuala ya siasa barani Afrika kwa mwaka 2012.

Kwa mujibu wa kampuni ya Microsoft kutoka Marekani inayojihusisha na masuala ya Kompyuta iliyoandaa tuzo hizo, Mdee na Kanza ni miongoni mwa viongozi jasiri katika masula ya siasa kutoka barami Afrika ambao wanahitaji kupongezwa.

“Mwaka 2012 ulikuwa mwaka mzuri kwa viongozi wanawake wa kisiasa pamoja na marais wawili wanawake na viongozi wawili wanawake kutoka Umoja wa Afrika, Microsofti iliangalia wanawake 11 ambao wako makini katika masuala ya siasa barani Afrika,” ilieleza sehemu ya maelezo yaliyowekwa kwenye mtandao.

Wengine waliotunukiwa ni Rais wa Malawi, Joyce Banda; Rais wa Liberia, Ellen Johnson Sirleaf; Mbunge kutoka Kenya, Charity Ngilu; Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wa Rwanda, Louise Mushikiwabo na Waziri wake wa Afya, Agnes Binagwaho.

Wengine ni Rais wa Muungano wa Afrika, Nkosa Zana Dlamini Zuma; Waziri wa Fedha wa Nigeria, Ngozi Okojo-Iweala; Makamu wa Rais wa Zimbabwe, Joyce Mujuru na Mwenyekiti wa chama cha CPPG cha Ghana, Samia Nkhrumah
CHANZO:EDDY BLOG
Share this article :

0 comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

KITULO FM LOGO

KITULO FM LOGO
Tusikilize masaa 18 kwa siku kupitia masafa ya 97.0 FM ukiwa wilayani Makete mkoani Njombe na maeneo ya jirani

WASOMAJI WETU

KUMBUKUMBU YA HABARI ZETU

 

Copyright © 2013. KITULOFM BLOG - Haki zote zimehifadhiwa
Imetengenezwa na Edwin Moshi
Inawezeshwa na Kitulo Fm