Home » » MKUU WA MKOA WA NJOMBE AKERWA NA UBOVU WA MADAWATI MADARASA YA AWALI

MKUU WA MKOA WA NJOMBE AKERWA NA UBOVU WA MADAWATI MADARASA YA AWALI

Written By kitulofm on Tuesday, 15 April 2014 | Tuesday, April 15, 2014





 MKUU WA MKOA AMELAANI KITENDO HIKI CHA MADAWATI KUHIFADHIWA VIBAYA MENGINE YAMEVUNJIKA NA KUWATAKA WAKUU WA SHULE KUYATUNZA MADAWATI HAYO
Mkuu wa mkoa wa Njombe keptain Mstaafu Aseri Msangi ameziagiza halmashauri za mkoa wa Njombe kutengeneza madawati kwaajili ya wanafunzi wa madarasa ya chekechea huku wananchi wakitakiwa kuchangia chakula shuleni ili kuboresha kiwango cha taaluma shuleni.

Akizungumza wakati wa kukagua mazingira ya shule ya msingi Ilunda    Mkuu wa mkoa  Keptain Mstaafu Aseri Msangi amewataka walimu kutunza samani zilizopo kwa kutengeneza ili kupunguza changamoto ya upungufu wa madawati inayozikabili shule nyingi za msingi mkoani Njombe.

Aidha Keptain Msangi amewapongeza wananchi wa kitongoji cha Lima kwale kwa ujenzi wa shule ya msingi Ilunda Mkondo B na kuwataka kukamilisha ujenzi wa madarasa na sehemu ya kupikia chakula cha wanafunzi huku akimuagiza mkurugenzi wa halmashauri ya Wilaya ya Njombe Paulo Malala kuhakikisha anapeleka mwalimu mkuu  wa kusimamia shule hiyo ili ifikapo july mwaka huu iweze kufunguliwa rasmi na kuanza masomo.

Katika hatua nyingine  Keptain Msangi amewaondoa hofu wananchi mkoani hapa juu ya matumizi ya mbolea aina ya minjingu  mazao  kwa kuwataka wananchi kuepukana na kilimo cha mazoea  na kwamba mbolea hiyo inafaa kwa kilimo cha mazao huku akitolea mfano shamba lake alilolima mwaka huu na kupandia mbolea hiyo katika kijiji cha Itipingi kuwa ametumia mbolea ya minjingu mazao na mahindi yameonekana kustawi vizuri.

Akisoma taarifa fupi mbele ya mkuu wa mkoa wa Njombe afisa mtendaji wa kijiji cha Ilunda bwana Yarabi Kafumbe amesema kuwa lengo la wananchi wa kijiji hicho kuanzisha shule hiyo ya mkondo B,Iliyopo kitongoji cha Limakwale katika shule ya msingi Ilunda ni kutaka kuwapunguzia wanafunzi kusafiri umbali mrefu kwani kwa sasa wanasafiri umbali wa kilomita takribani tano.

Aidha bwana Kafumbe amesema kuwa madarasa ya shule hiyo yamegharimu shilingi milioni kumi na tatu na laki tatu ambapo halmashauri ya wilaya ilichangia shilingi milioni  kumi na moja na wananchi wakichangia shilingi milioni mbili na laki tatu huku akiwaomba wadau wa elimu kusaidia kuchangia ujenzi huo ili kuendelea kuboresha vyumba vingine vya madarasa na ofisi.

Ziara hiyo ya siku tatu ya  Mkuu wa mkoa wa Njombe imelenga   kukagua utekelezaji wa miradi ya maendeleo wilayani Hapa ambapo Jumla ya shilingi laki nne zimeahidiwa na mkuu huyo wa mkoa kwaajili ya kutengeneza madawati ya wanafunzi wa darasa la chekechea katika shule ya msingi Ilunda mkondo B ambayo yanalingana na umri wao ambapo leo ziara hiyo inaendelea kwa vijiji vya taraafa ya Lupembe.
 
Share this article :

0 comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

KITULO FM LOGO

KITULO FM LOGO
Tusikilize masaa 18 kwa siku kupitia masafa ya 97.0 FM ukiwa wilayani Makete mkoani Njombe na maeneo ya jirani

WASOMAJI WETU

KUMBUKUMBU YA HABARI ZETU

 

Copyright © 2013. KITULOFM BLOG - Haki zote zimehifadhiwa
Imetengenezwa na Edwin Moshi
Inawezeshwa na Kitulo Fm