Majirani wakimuhudumia majeruhi ndani ya gari.
Katika hali isiyokuwa ya kawaida mtu mmoja aliyefahamika kwa jina la
London Haonga(61) mkazi wa Kijiji cha Mapogolo Kata ya Mbebe Wilaya ya
Ileje Mkoani Mbeya amejeruhiwa vibaya kwa kukatwa nyeti zake na watu
watatu wasiofahamika kisha kutokomea nazo kusikojulikana.
Tukio hilo limetokea majira ya saa mbili usiku April 19 mwaka huu
baada ya mmoja kati ya watuhmiwa kufika nyumbani kwa mzee huyo kisha
kubisha mlango akiomba msaada wa kuonyeshwa njia akidai amepotea njia.
Mzee London alipotoka nje ya nyumba akiwa anamwelekeza njia mtu huyo
anayedaiwa kuwani mjukukuu wake mita chache kutoka nyumbani kwake
alifunikwa na kitambaa usoni na watu wawili kisha kuangushwa na kukatwa
nyeti zake ambazo waliondoka nazo.
Mtendaji wa Kijiji cha Mapogolo Cosmas Haonga amesema baada ya unyama
huo Mzee London alipoteza fahamu na alipozinduka alipiga yowe kuomba
msaada ambapo majirani walifika na kutoa msaada wa kumkimbiza Hospitali
ya Wilaya ya Ileje huku wakiwasaka watuhumiwa wa tukio hilo.
Kwa mujibu wa Mtendaji wa Kijiji imedaiwa kuwa watuhumiwa wa tukio
hilo wanatokea Mpemba wilaya ya Momba ambao walitambuliwa na mhanga wa
tukio hilo ambapo baada ya kupewa PF 3 mzee London amekimbizwa Hospitali
ya Rufaa Mbeya ambapo alifikishwa Hospitali ya Rufaa majira ya saa
11:00 jioni April 20 huku akilalamika kwa maumivu makali.
Kwa upande wake Kamanda wa Polisi Mkoani Mbeya Ahmed Msangi
amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kudai kuwa chanzo cha awali
imedaiwa sababu za kutendewa ukatili huo umetokana na mmoja wa ndugu
aliyedai kuwa mzee huyo anatuhumiwa kuwa na mahusiano ya kimapenzi na
mke wa mdogo wake hivyo watu hao walitumwa kwa nia ya kulipiza kisasi.
Aidha imedaiwa kuwa baadhi ya viungo vimekamatwa na wengine kudai
kuwa tukio hilo kuhusishwa na imani za kishirikina kwani imedaiwa
watuhumiwa kuimbilia nchi jirani mara baada ya kutenda kitendo hicho cha
kikatili.
Kamanda Msangi ameoa wito kwa jamii kuacha tabia za kujichukulia
sheria mkononi amesema pindi wanapokuwa na migogoro ni vema kutatua
migogoro kwa njia ya mazungumzo ili kuleta amani na kuahidi wale wote
waliohusika na tukio hili wanakamatwa na kufikishwa kwenye mikono ya
sheria kwani hakuna mtu aliye juu ya sheria.
(Habari/Picha: Ezekiel Kamanga wa Mbeya Yetu Blog)
0 comments:
Post a Comment