Baada ya siku chache
kugundulika kuwa Mwl.Mkuu wa shule ya Msingi Unenamwa kata ya Luwumbu wilayani
Makete Mkoani njombe anauza pombe za kienyeji na viwandani kwenye nyumba ya shule
hiyo hali hiyo imethibitishwa leo na wananchi wa kijiji hicho
Wakizungumza katika
mkutano uliofanywa na Mratibu wa Elimu kata ya Luwumbu Bw.Burton Mbedule
wamesema kuwa ni kweli Mwl.Mkuu wa shule ya Msingi Unenamwa Evaristo Maginga
amefungua kisiri kilabu cha kuuza Pombe za kienyeji na viwandani katika nyumba
ya shule hiyo
Katika Mkutano huo mratibu
elimu kata Bw.Mbedule aliwataka wananchi wa kijiji hicho kumthibitishia taarifa
hizo kama ni kweli kwani amesema yeye aliposikia taarifa hiyo alimuona
Mwenyekiti na kuzungumza naye kuhusu uvumi huo,baada ya hapo alikutana na
mwalimu huyo ambapo alimwambia mratibu huyo kuwa anataka anataka uthibitisho wa
watu waliokuwa wanapata huduma hiyo kwake
Baada ya hapo amesema
aliwatafuta wananchi kabla ya kuitisha Mkutano huo ambapo wananchi walimweleza
kuwa taarifa za mwl.huyo kutengeneza pombe ni kweli na si kuuza pombe eneo la
shule
Bw.Mbedule Alipowataka
wananchi kumthibitishia taarifa hizo katika Mkutano huo uliokuwa chini ya
Mwenyekiti wa kijiji Bw.Labson Tweve wananchi wamesema kuwa huwa wanajipatia
huduma hiyo katika nyumba hiyo hata kwa Oda na sio uongo kwamba huduma hiyo
haipo shuleni hapo kwani wamekuwa wakiipata nyumbani hapo
Akizungumza na Kitulo
fm Mwl. huyo siku ya Alhamisi wiki iliyopita katika kipindi cha Morning power
alikana taarifa hizo na kusema kuwa kuwa yeye anauza vitu vidogovidogo na si
Pombe
Hata hivyo wazazi wa
watoto wanaosoma katika shule ya Msingi Unenamwa wameeleza kukerwa na elimu duni
itolewayo na walimu waliopo shuleni hapo kwani wamekuwa wakikagua madaftari ya
watoto wao na kusema ni tofauti na wanafunzi wanaosoma katika shule jirani kama
Idende
Hivyo baadhi yao
wamelazimika kuwahamisha watoto wao katika shule hiyo na kuwapeleka shule
nyingine ya Idende kwa kuhofia watoto wao kupata elimu Duni kwani endapo wakipelekwa Sekondari watakuwa na
Uelewa Mdogo
Baadhi ya wananchi wa
kijiji hicho wamesema hawajapendezwa na tabia ya walimu wa shule hiyo kwani
wanafunzi wamekuwa wakifanya vibarua muda wa masomo kutoka Unenamwa hadi
Mwakavuta kitu ambacho kinaongeza kufeli kwa wanafunzi kitaaluma
Hatma ya Mkutano huo
wananchi wamemtaka Mratibu Elimu wa kata hiyo kuzungumza na Mwl.huyo na
kumuonya mara moja aache biashara hiyo katika eneo la shule.
Na Furahisha Nundu
0 comments:
Post a Comment