Home » » ASIMULIA BABA YAO MZAZI ANAVYOWABAKA

ASIMULIA BABA YAO MZAZI ANAVYOWABAKA

Written By kitulofm on Wednesday, 27 November 2013 | Wednesday, November 27, 2013

Moshi. Katika hali isiyo ya kawaida, mwanamme mmoja mkazi wa Kijiji cha Kiria, Kata ya Mamba Kusini, Wilaya ya  Moshi, Mkoa wa Kilimanjaro, anadaiwa kuwabaka na kuwaingilia kinyume cha maumbile watoto wake wawili wenye umri wa miaka 10 na 13 na kuwajeruhi vibaya.

 Mwandishi alivyofuatilia
Ni saa 7:30 mchana nafika nyumbani kwa mwanamme huyo anayetajwa na baadhi ya watu hapa Moshi kwamba anawabaka watoto wake.Nabisha hodi, sipati wa kunijibu, baadaye anatokea jirani na kuniambia wenyewe hawapo,  namweleza kilichonileta na anakuwa tayari kunisaidia.
Jirani huyo ananipeleka kwa msamaria mwema anayemtunza mtoto wa miaka 13 aliyefanyiwa ukatili na baba yake mzazi kwa kubakwa na kulawitiwa kwa zaidi ya miaka miwili na nusu sasa nikiwa njiani anasema “Unapomwangalia mtoto huyo huwezi amini kuwa kitendo hiki kimetendwa na baba mzazi ambaye bila shaka  kabla ya kuwa na watoto aliomba kwa Mungu na alitamani  sana kuwa na watoto naye aitwe baba”
Nafika kwa msamaria huyo katika Kijiji cha Kiria, Kata ya Mamba Kusini, najitambulisha na kumweleza lengo langu, ananyanyuka na kuingia ndani kuzungumza na mtoto anarudi na jibu lililonipa uchungu na kunitoa machozi.

 Anamtaja mtoto jina na kusema amesema hataki kuongea na mwanamme, kama unataka mwambie huyo mwanamme atoke hapo nje. Mwanaume anayezungumziwa ni yule ambaye alinisindikiza kuja hapo kumwona.
Ilinilazimu  nimwambie mtu huyo niliyekuwa naye aondoke ili nipate nilichofuata kijijini hapo.
Baada ya kuondoka, mtoto huyo akiwa na uso wa majonzi alitoka nje na kunisalimia kisha kukaa na kuanza kunieleza mateso na ukatili wa kutisha aliofanyiwa na baba yake mzazi.
Mateso kutoka kwa baba
Mtoto huyo anasema hakumbuki siku ambayo baba yake alianza kumbaka lakini anasema ni siku nyingi; mara baada ya baba yake kutengana na mama yao, zaidi ya miaka miwili iliyopita.
Anasema baba yake huyo alianza kufanya unyama huo kwa mdogo wake ambaye sasa ana miaka kumi na baadaye akaanza kumwingia na yeye na kwamba alikuwa akifanya kwa zamu huku akiwafunga midomo ili wasipige kelele.
Anasema mara zote alipowafanyia unyama huo alikuwa na panga pembeni akiwatishia kuwachinja kama watakataa au kusema kwa mtu yeyote.
Mtoto huyo anaeleza kuwa baba yao alioa mke mwingine, lakini bado akawa anawaingilia, ndipo siku moja mwanamke huyo alipomfumania na kupigana nae sana kabla ya kuamua kuondoka na kuachana naye.
Share this article :

0 comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

KITULO FM LOGO

KITULO FM LOGO
Tusikilize masaa 18 kwa siku kupitia masafa ya 97.0 FM ukiwa wilayani Makete mkoani Njombe na maeneo ya jirani

WASOMAJI WETU

KUMBUKUMBU YA HABARI ZETU

 

Copyright © 2013. KITULOFM BLOG - Haki zote zimehifadhiwa
Imetengenezwa na Edwin Moshi
Inawezeshwa na Kitulo Fm