Home » » DK MVUNGI AFARIKI DUNIA

DK MVUNGI AFARIKI DUNIA

Written By kitulofm on Wednesday, 13 November 2013 | Wednesday, November 13, 2013

wehu
MJUMBE wa Tume ya 

Mabadiliko ya Katiba aliyekuwa akipatiwa matibabu nchini Afrika Kusini Dk. Sendongo Mvungi amefariki dunia.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Katibu wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba Assaa Rashid jana jioni  alisema Dk.Mvungi alifariki saa  8:30 mchana kwa saa za Afrika ya Kusini akiwa katika Hospitali ya Milpark.
“Kwa masikitiko makubwa,Tume inawafahamisha wananchi kuwa Mjumbe wake, Dkt. Sengondo Mvungi aliyekuwa akipata matibabu katika Hospital ya Milpark iliyopo jijini Johannesburg nchini Afrika Kusini amefariki dunia leo(jana),”alisema.
Rashid katika taarifa yake fupi ya awali alisema :”Taratibu za kuusafirisha mwili wa marehemu kutoka nchini Afrika Kusini kuja nchini kwa mazishi zinaendelea na taarifa zaidi zitatolewa kesho(leo)”.
Marehemu Dk. Mvungi alisafirishwa siku ya Alhamisi, Novemba 7, mwaka huu kwenda nchini Afrika Kusini kwa uchunguzi na matibabu zaidi akitokea Kitengo cha Mifupa Muhimbili (MOI) aliokuwa amelazwa baada ya kuvamiwa nyumbani kwake Kibamba, jijini Dar es Salaam na watu waliomjeruhi vibaya kichwani usiku wa kuamkia siku ya Jumapili, Novemba 3, 2013.
Katika taarifa hiyo, Tume pia imewaomba watanzania wote kuungana na familia, ndugu, jamaa na marafiki wa marehemu Dk. Mvungi katika kuomboleza msiba huo.
Share this article :

0 comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

KITULO FM LOGO

KITULO FM LOGO
Tusikilize masaa 18 kwa siku kupitia masafa ya 97.0 FM ukiwa wilayani Makete mkoani Njombe na maeneo ya jirani

WASOMAJI WETU

KUMBUKUMBU YA HABARI ZETU

 

Copyright © 2013. KITULOFM BLOG - Haki zote zimehifadhiwa
Imetengenezwa na Edwin Moshi
Inawezeshwa na Kitulo Fm