Wanafunzi wa shule ya
sekondari Lupalilo iliyopo wilayani Makete wameelezea kupanda kwa kiwango cha
Taaluma kwa wanafunzi shuleni hapo
Wakizungumza na kitulo fm
katika kipindi cha skuli club kinachorushwa kila siku ya juma mosi saa
1:15usiku-2:00 usiku ambapo wamesema kuwa kiwango cha ufaulu kwa
wanafunzi umeongezeka kutoka
asilimia 65-kufikia 90 kulingana na jitihada za walimu pamoja na kujisomea
wanafunzi wenyewe pindi wanapokuwa shuleni na majumbani
Wakizungumzia suala la baadhi
ya wanafunzi wa kike kupata mimba wawapo shuleni wamesema kuwa baadhi ya shule
mazingira wa wanafunzi wa kike kuishi nje ya bweni ni moja ya sababu
zinazofanya mwanafunzi kupata mamba
Hata hivyo wamewataka
wanafunzi wengine nchini kujikinga na suala hilo na kupunguza utoro shuleni ili kuongeza
kiwango cha elimu wilayani hapa na nchi nzima
0 comments:
Post a Comment