Home »
» MAADHIMISHO YA SIKU YA CHOO DUNIANI MKOANI MWANZA.
Mila
potofu zimetajwa kuchangia kwa asilimia kubwa maambukizi ya maradhi
yatokanayo na kukiuka kanuni za afya na usafi, likibainika katika
utafiti uliofanywa kwa wakazi wa vijiji vya wilaya ya Magu, ambapo
familia moja yenye zaidi ya watu kabla ya kula, hunawa maji kwenye
bakuli moja kasha mara baada ya hapo mzee wa familia huyanywa maji hayo
kama tiba ya kutanua kifua au humnywesha motto mchanga kwa makusudi hayo
ya kumpanua kifua.
Takwimu
za vyoo katika jiji la mwanza zinaonyesha kuwa vyoo bora ni asilimia
64%, vyoo duni ni asilimia 33% na nyumba ambazo hazina vyoo kabisa ni
asilimia 3%, changamoto ya tatizo hilo ikitajwa kuwa ni pamoja na
gharama kubwa ya vifaa vya ujenzi, umasikini na ufukara wa wananchi
kutokana na kipato duni na kiwango cha uelewa,na hali ya miamba na
baadhi ya maeneo kuwa na chemichemi nyingi hasa mabondeni.
Kwa upande wa matumizi ya vyoo kulingana na hali ya kijiografia na
jinsi ujenzi holela milimani ulivyo, imegundulika kuwa siyo kwamba
nyumba zote zilizoko sehemu za milima hazina vyoo bali taarifa sahihi ni
kwamba vyoo vilivyopo maeneo hayo siyo bora na si vya kudumu.
Sambamba
na maadhimisho hayo ambayo yamefanyika kwa kila halmashauri nchini huku
mkoa wa Tanga yakifanyika kitaifa , halmashauri ya jiji la Mwanza kwa
kushirikiana na PLAN INTERNATIONAL imefanya maonesho katika viwanja vya
furahisha ya choo rahisi bora na cha kisasa kama darasa kwa wananchi.
0 comments:
Post a Comment