Home » » MTENDAJI WA KIJIJI CHA MLONDWE MAKETE ALAMBA FEDHA ZA SERIKALI NA KUKIMBILIA KUSIKOJULIKANA

MTENDAJI WA KIJIJI CHA MLONDWE MAKETE ALAMBA FEDHA ZA SERIKALI NA KUKIMBILIA KUSIKOJULIKANA

Written By kitulofm on Friday, 1 November 2013 | Friday, November 01, 2013

MKURUGENZI MTENDAJI HALMASHAURI YA WILAYA YA MAKETE IDDI NGANYA
Mtendaji wa kijiji cha mlondwe ametoweka katika eneo lake la kazi baada ya kukiri kutumia vibaya mchango wa wananchi wa ujenzi wa nyumba ya mwalimu mbela na kisaula

Mtendeji huyo Bw.omari mkwama ambaye anadaiwa kukiri kurudisha kiasi cha shiringi laki sita na elfu arobaini na sita za mchango huo ambazo aliahidi kurudisha tarehe 08/10 mwaka huu ,hali hiyo imebainishwa na diwani wa kata hiyo wakati wa uwasilishaji wa taarifa ya utekelezaji wamaendeleo katika kata yake

Naye mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya makete bw.idd nganya amekiri kupokea kwa taarifa ya mtendaji huyo na kwamba hatua zitachukuliwa na kuongeza kuwa serikali ya kijiji na kata inatakiwa kushitaki mahakamani kwa matumizi mabaya ya fedha za wananchi.
Share this article :

0 comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

KITULO FM LOGO

KITULO FM LOGO
Tusikilize masaa 18 kwa siku kupitia masafa ya 97.0 FM ukiwa wilayani Makete mkoani Njombe na maeneo ya jirani

WASOMAJI WETU

KUMBUKUMBU YA HABARI ZETU

 

Copyright © 2013. KITULOFM BLOG - Haki zote zimehifadhiwa
Imetengenezwa na Edwin Moshi
Inawezeshwa na Kitulo Fm