KITUO cha Sheria na Haki za Binadamu
(LHRC) kimemtaka Naibu Waziri wa Nishati na Madini, George Simbachawene,
kuwaomba radhi Watanzania kutokana na kutoa kauli ya kukatisha tamaa.
Simbachawene, juzi alitoa kauli ya
serikali ya kupandisha bei ya umeme kama Shirika la Umeme Tanzania
(TANESCO), lilivyoomba hivi karibuni kutaka kuongeza gharama za nishati
hiyo kwa asilimia 68.
Alisema ni ukweli usiopingika kuwa hata TANESCO ikiongeza gharama za
umeme hadi kufikia sh 800 kwa uniti bado bei hiyo itaendelea kuwa nafuu
ukilinganisha na gharama za kununua mafuta ya taa.
SOMA ZAIDI.TANZANIA DAIMA
0 comments:
Post a Comment