Home » » MMOJA AJERUHIWA NA NYATI KIJIJI CHA ILEVELO WILAYANI MAKETE

MMOJA AJERUHIWA NA NYATI KIJIJI CHA ILEVELO WILAYANI MAKETE

Written By kitulofm on Monday, 18 November 2013 | Monday, November 18, 2013


MAKETE

Mtu mmoja mkazi wa kijiji cha Ilevelo kata ya Lupalilo Bw.Alfred Sanga amejeruhiwa  na mnyama anayesadakiwa kuwa ni nyati hii leo majira ya saa 3 asubuhi kijijini hapo

Akihibitisha kutokea kwa tukio hilo M/kiti wa kijiji hicho Bw.Festo Mahenge amesema kuwa tukio hilo limetokea mnamo saa 3 asubuhi wakati Bw.Alfred sanga akiwa anaelekea machungoni kwa ajili ya kuangalia Ng’ombe wake ndipo alipomkuta mnyama huyo aina ya nyati akiwa amelala na ghafla alizinduka na kumjeruhi eneo la shingo yake

Amesema majeruhi huyo alipata nafasi ya kukimbia na ndipo akapelekwa Hospitali ya Mission ya Ikonda iliyopo kata ya Tandala wilayani Makete kwa matibabu zaidi,imeelezwa kuwa amehudumiwa na kuruhusiwa kurudi nyumbani kwake ambapo hali yake hadi hivi sasa inaendelea vizuri

Hata hivyo M/kiti wa kijiji hicho Bw.Mahenge amesema kuwa ni hali ya kushangaza kutokea kwa mnyama huyo kijijini hapo kwani ni mara ya kwanza ambapo amesema kuwa mnyama huyo inasadikika ametokea mpakani mwa kijiji jirani cha Mago na Ugabwa

Pia ametoa wito kwa wakazi wa kijiji hicho kuchukua tahadhari wakati wakiwa wakitembea popote kwani hiki ni kipindi cha mavuno ya ngano na kupanda viazi mashambani hivyo kuwa katika makundi kwani kuna dalili za kuwepo kwa mnyama huyo mazingira hayo
Share this article :

0 comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

KITULO FM LOGO

KITULO FM LOGO
Tusikilize masaa 18 kwa siku kupitia masafa ya 97.0 FM ukiwa wilayani Makete mkoani Njombe na maeneo ya jirani

WASOMAJI WETU

KUMBUKUMBU YA HABARI ZETU

 

Copyright © 2013. KITULOFM BLOG - Haki zote zimehifadhiwa
Imetengenezwa na Edwin Moshi
Inawezeshwa na Kitulo Fm