Home » » NSSF KUTOA MIKOPO YA MILIONI 869.11 KWENYE SACCOS 7 NJOMBE

NSSF KUTOA MIKOPO YA MILIONI 869.11 KWENYE SACCOS 7 NJOMBE

Written By kitulofm on Friday, 1 November 2013 | Friday, November 01, 2013

 
 
Na Gabriel  Kilamlya Njombe
 
Jumla ya Mkopo wa Shilingi Milioni 175 Unatarajiwa Kutolewa Kwa Wachama wa NSSF Mkoa wa Njombe Kupitia SACCOS  ya Lupembe na Wafanyabiashara Njombe  Saccos Katika Siku Zijazo Ili Kuwaboreshea Biashara na Uchumi wa Wananchi Mkoani Hapa.

Kutolewa Kwa Mkopo Huo Katika Saccos Mbili Kwa Kipindi cha Hivi Karibuni Kitapelekea Kuwepo kwa Jumla ya Shilingi Milioni 869.11 Kwa Jumla ya Saccos Saba Ndani ya Mkoa wa Njombe.
 
Akizungumza na Kituo Hiki Meneja wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii NSSF Mkoa wa Njombe Bwana Godwin Mwakalukwa Amesema Kuwa Saccos za Mkoa wa Njombe Zimeonesha Mwitikio Mzuri Katika Kujitokeza Kuomba Mkopo Kwa ajili ya Kuwasaidia Wanachama Wake Tofaoti na Mikoa Mingine Nchini.

Bwana Mwakalukwa Amesema Kuwa Suala la Uhamasishaji Linalofanywa na NSSF Mkoa wa Njombe Limepelekea Saccos Nyingine Kuonesha Nia ya Kuomba Mikopo Katika Kuhakikisha Wanachama Wake Wananufaika na Mikopo Hiyo Inayotolewa Kwa Riba Ndogo ya Asilimia 9 Hadi 10 Kulingana na Ukubwa wa Mkopo.

Pamoja na Mambo Mengine Amesema Kuwa Baadhi ya SACCOS Tayari Wameanza Kurejesha Mikopo yao Hali Inayopelekea Kujenga Uaminifu wa Kuweza Kupata Mkopo Mwingine.

Hivi Karibuni NSSF Mkoa wa Njombe Imetoa Jumla ya Shilingi Milioni 250 Katika Saccos Ya Nyombo Ambapo Wanachama Wake Watakaonufaika na Mkopo Huo ni Wale Waliojiunga na NSSF Pekee.


Na Kabriel Kilamlya
Share this article :

0 comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

KITULO FM LOGO

KITULO FM LOGO
Tusikilize masaa 18 kwa siku kupitia masafa ya 97.0 FM ukiwa wilayani Makete mkoani Njombe na maeneo ya jirani

WASOMAJI WETU

KUMBUKUMBU YA HABARI ZETU

 

Copyright © 2013. KITULOFM BLOG - Haki zote zimehifadhiwa
Imetengenezwa na Edwin Moshi
Inawezeshwa na Kitulo Fm