WAZIRI Mkuu, Mizengo Pinda, amewataka maofisa mipango miji nchini
kurekebisha utendaji wao wa kazi ili waweze kubadili taswira mbaya
iliyojengeka miongoni mwa jamii dhidi yao.
Pinda alitoa kauli hiyo jana wakati akifungua mkutano wa kwanza wa wataalamu wa Mipangomiji waliosajiliwa na Bodi ya Usajili wa Wataalamu wa Mipangomiji Dar es Salaam.
“Taswira ya utendaji kazi katika taaluma ya mipangomiji na katika sekta ya ardhi kwa ujumla miongoni mwa wananchi na serikali sio nzuri sana.
Watafiti wanatueleza kuwa kati ya asilimia 60 na 80 ya makazi kwenye miji yetu hapa nchini yamejengwa kiholela. Na kwa kiwango hicho hicho wakazi wa mijini wako kwenye makazi hayo na wanaishi kiholela.
“Wako wanaosema ninyi ndiyo chanzo cha hiyo migogoro, wako wanaosema ninyi kwa rushwa ndiyo wenyewe, mimi sishangai madai haya ila ninawasihi muwe na roho ngumu katika kushinda vishawishi hivi,” alisisitiza.
Aliwataka wajadili masuala yanayohusu migogoro ya ardhi baina ya wafugaji na wakulima, baina ya mipaka ya vijiji, baina ya wilaya, baina ya wanavijiji na hifadhi za taifa au maeneo ya uchimbaji madini na kujadili njia za kutatua migogoro hiyo ili kuwa na mipamgo endelevu.
Aliwataka waangalie suala la ukuaji wa miji iliyo karibu na Jiji la Dar es Salaam kwa kuangalia dhana ya miji mikubwa kubeba vijiji vinavyoizunguka, hasa kuangalia uwezekano wa kupunguza mrundikano wa watu katika jiji hilo.
“Miji ya Kibaha, Mkuranga na Bagamoyo inatumikaje kusaidia kupunguza msongamano katika Jiji la Dar es Salaam?” alihoji Pinda.
Alisema wataalamu wa mipangomiji wanapaswa kuwa na maono makubwa ya baadaye kama kweli wanataka kupunguza majanga katika siku za usoni.
“Angalieni utafiti wa gesi unaoendelea pale Mtwara na mjipange, angalieni mpango wa ujenzi wa Bandari ya Bagamoyo na kuunganisha na Reli ya Kati, angalieni Lindi na upatikanaji wa Liquefied Natural Gas (LNG), pangeni miji kwa siku za baadaye si sasa,” alisisitiza.
Aliwataka wanataaluma hao wasimamie vema taaluma yao kwani katika miaka 37 ijayo (mwaka 2050) inakadiriwa kwamba nusu ya watu wote watakuwa wakiishi mijini.
Awali, Waziri wa Ardhi na Maendeleo ya Makazi, Profesa Anna Tibaijuka, alisema maofisa mipango miji wanakabiliwa na changamoto ya kufikiri na kubuni aina ya miji ambayo itakidhi mahitaji ya jamii ya baadaye.
Alisema hata hivyo maofisa hao wamekuwa wakikabiliwa na changamoto ya kushindwa kutoa uamuzi ama ushauri wa kitaalamu kwa kuhofia kuadhibiwa na madiwani.

0 comments:
Post a Comment