Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limetupilia mbali ombi la Umoja wa Afrika kutaka kuahirishwa kwa mwaka mmoja kesi dhidi ya Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta, na naibu wake William Ruto, katika mahakama ya ICC.
Ombi la serikali ya Kenya la kutaka kuahirishwa kwa kesi hiyo ya uhalifu halikukubalika baada ya wanachama 7 kati ya 15 waliopiga kura kukataa ombi hilo.
Nchi nane wanachama wa baraza hilo hazikushiriki katika zoezi hilo.
Angalau kura takriban tisa zilihitajika ili kupita kwa azimio hilo lililotolewa na Umoja wa Afrika.
CHANZO dwkiswahili
0 comments:
Post a Comment