KUNDI la wafugaji wakiwa na mifugo yao, wameendelea kuwatesa wakulima
wa Wilaya ya Namtumbo mkoani Ruvuma kwa kulisha mifugo yao kwenye
mashamba ya mihogo, zao ambalo ni tegemeo kubwa kwa wananchi wa wilaya
hiyo.
Akizungumza kwa masikitiko, Allen Ngongole mkulima wa Kijiji cha
Ligera, alisema kuwa, mpaka sasa amepoteza ekari moja ya shamba la
mihogo kutokana na kuharibiwa na mifugo na kumfanya aishi porini kwa
kulinda mashamba mengine yasiharibiwe na mifugo hiyo.
Zao aina ya Mtama
Diwani wa Kata
ya Ligera, Ally Ndauka alipohojiwa kwa njia ya simu kuhusu kuwepo kwa
mifugo hiyo, alikiri kuwepo kwa mifugo hiyo, licha ya jitihada zake
za kuwataka wafugaji hao kuondoka katika maeneo yake na kuelekeza
lawama kwa viongozi na wananchi wa vijiji vya kata yake kuwakumbatia
wafugaji hao.
Ndauka aliongeza kuwa, aliwasilisha taarifa ya kuwaondoa wafugaji
katika kata yake kwenye mkutano wa maendeleo ya kata, pamoja na mambo
mengine, aliwataka viongozi wa vijiji na watendaji kushirikiana
kuwaondoa wafugaji katika maeneo yao na kupisha shughuli za kilimo,
taarifa ambayo ilipingwa vikali na wajumbe wa mkutano huo.
Akizungumza kwenye kikao cha Baraza la Madiwani hivi karibuni Mkuu
wa Wilaya hiyo, Abdul Lutavi aliwaagiza madiwani kuhakikisha kwamba,
wanawaondoa wafugaji hao katika maeneo yao na kupisha shughuli za
kilimo.
“Hakuna maeneo yaliyotengwa katika wilaya yangu kwa ajili ya
wafugaji pekee, hivyo kuendelea kubaki na kundi kubwa la wafugaji ni
kukaribisha vurugu dhidi ya wakulima,“ alisema mkuu wa wilaya huyo.
Baadhi ya wafugaji ambao hawakutaka kutaja majina yao, walisema kuwa,
wapo katika maeneo hayo baada ya kukubaliwa na serikali za vijiji
kuendelea na hsughuli zao.
Maeneo yaliyoathirika sana na wafugaji hao katika Wilaya ya Namtumbo ni Kata ya Mkongo, Ligera, Lusewa na Magazine
0 comments:
Post a Comment