Jamii imetakiwa kushirikiana
na wadau mbalimbali ili kutokomeza suala
la unyanyasaji wa kijinsia pamoja na ukatili dhidi ya wanawake.
Hayo yamesemwa kwenye
kipindi cha hazina ya mwanamke kinachorushwa na
kitulo fm kila siku ya jumapili saa mbili na 15 hadi saa tatu na 15
usiku na mtangazaji Veronica Mtauka(Super mama)
Mtangazaji Veronica Mtauka
katika kipindi hicho cha hazina ya mwanamke aliweza kuzungumza na Fatuma Himili kutoka dawati la jinsia kituo cha polisi Makete ambapo msimamizi wake ni WP Fatuma Himili kwa kata ya iwawa amesema kuwa wao kama dawati la jinsia wanakutana na changamoto mbalimbali ikiwemo wanawake kushindwa kutoa ushirikiano wa kuweza kuwafikisha wanaotenda ukatili dhidi ya wanawake katika vyombo vya sheria kama mahakamani

Hata hivyo alikuwepo Bi. Monica
Hindi kuto katika shirika la pamoja tuwalee (ELCT) lililopo wilayani hapa na makazi yao makuu yapo katika kata ya Iwawa Makete mjini amesema kazi yao kubwa ni kutoa elimu kwa jamii ili
kutokomeza ukatili zidi ya wanawake na watoto kuanzia vijiji hadi mjini.
Na Veronica Mtauka
0 comments:
Post a Comment