WATU
wanne wamepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu,
wakikabiliwa na mashitaka ya kuwa wanachama wa kundi la kigaidi la Al
Shabaab. Washitakiwa hao waliofikishwa mahakamani jana ni Ally Rashid,
Shaban Waziri, Faraji Ramadhani na Mussa Mtweve.
Wakili
wa Serikali, Peter Maugo alidai mbele ya Hakimu Mkazi Sundi Fimbo, kuwa
kati ya Januari 11 mwaka jana na Septemba 16 mwaka huu, eneo la
Kibaoni, Dar es Salaam, Rashid alisajili washitakiwa wenzake kuwa
wanachama wa kundi hilo.
CHANZO:HABARI LEO
0 comments:
Post a Comment