Home » » KILIMO MAKETE CHAZIDI KUKUA

KILIMO MAKETE CHAZIDI KUKUA

Written By kitulofm on Friday, 6 December 2013 | Friday, December 06, 2013

 Katibu mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na wananchi waliofika kushuhudia akikabidhi trekta la kulimia alilolikabidhi kwa vijana wa kata ya kigala tarafa ya ikuwo wilayani Makete hii leo

 
 Katibu mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akikabidhi funguo za trekta kwa mojawapo wa kijana wa kata ya Kigala wilayani Makete
Mbunge wa jimbo la Makete ambaye pia ni naibu waziri wa maji Dkt. Binilith Mahenge akizungumza katika mkutano huo wa CCM
======
Chama cha Mapinduzi (CCM) kimesema kitaendelea kufanya kazi na vijana wote bila kujali itikadi ya vyama vya siasa walivyonavyo kwa kuwa chama hicho kilipoomba ridhaa ya kuongoza nchi kiliahidi kuboresha maisha kwa watanzania wote

Kauli hiyo imetolewa na katibu mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana wakati akikabidhi trekta kwa vijana wa kijiji cha Mlengu kata ya Kigala wilayani Makete hii leo

Ndugu Kinana amesema trekta hilo limetolewa na chama cha mapinduzi ikiwa ni utekelezaji wa ilani ya CCM ya kuhakikisha wanaiboresha sekta ya kilimo hasa kwa vijana wakiwemo vijana wa Makete

Amewataka vijana hao kuendelea kuongeza zaidi kasi ya kilimo kwani ni njia mojawapo ya kujikwamua kiuchumi, huku akiwasisistiza kulitunza trekta hilo ili liweze kudumu

Vijana hao zaidi ya 200 wa kata ya Kigala tarafa ya Ikuwo wameandaa shamba la zaidi ya hekari 300 ambapo kupatiwa trekta hilo lenye jembe na haro litasaidia kuinua shughuli za kilimo kwa vijana hao

Wakati huo huo mbunge wa jimbo la Makete ambaye pia ni naibu waziri wa maji Dkt. Binilith Mahenge ameahidi kuwanunulia vijana hao tela la trekta hilo kwa kuwa linahitajika hasa kwa kubebea mazao yao na vitu vingine mashambani

Ameyasema hayo wakati akielezea shughuli zinazofanywa na serikali kutekeleza ilani ya CCM katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye viwanja vya ofisi ya CCM kijiji cha Mlengu

Ndugu Kinana ameambatana na katibu wa NEC itikadi na uenezi Nape Nnauye, katibu wa NEC siasa na uhusiano wa kimataifa na mbunge mteule Dkt. Asharose Migiro, viongozi mbalimbali wa chama na serikali wa mkoa wa Njombe na wilaya ya Makete
Share this article :

0 comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

KITULO FM LOGO

KITULO FM LOGO
Tusikilize masaa 18 kwa siku kupitia masafa ya 97.0 FM ukiwa wilayani Makete mkoani Njombe na maeneo ya jirani

WASOMAJI WETU

KUMBUKUMBU YA HABARI ZETU

 

Copyright © 2013. KITULOFM BLOG - Haki zote zimehifadhiwa
Imetengenezwa na Edwin Moshi
Inawezeshwa na Kitulo Fm