Elimu hiyo imejiri baada ya madereva pikipiki(bodaboda) hao kuandamana bila kibali kutokea eneo la dombwela kuelekea mtaa wa mabehewani ambapo kambi ilitua hapo na elimu ikaanza kutolewa kutoka kwa maaskari wa Usalama barabarani wilayani Makete
Katika hali hiyo madereva bodaboda hao wamedai kutozwa faini kubwa huku wakilalamika biashara kuwa ngumu na mazingira hayaruhusu kupata kiwango kikubwa cha fedha ukilinganisha na kiasi anachotozwa na Askari wa usalama Barabarani
Akiwaeleza kuhusu gharama hizo Askari aliyetambuliwa kwa jina la Afande Maiko amesema ni lazima dereva anapokuwa barabarabi afuate sheria za barabaraawe na leseni,chombo chake kuwa imara ndipo faini hizo zitaepukika
Amesema askari anapokusimamisha barabarani ni lazima akuelimishe kulingana na makosa uliyonayo pindi unapokuwa na kosa au kutokuwa na leseni ya udreva na si kukutoza faini wakati hujaelimishwa kuhusu miongozo ya sheria za barabarani
Hata hivyo Katibu wa chama cha Madereva bodaboda Makete mjini Bw.Emmanuel Alas akizungumza kwa niaba ya madereva hao amewaomba madereva hao kukutana siku ya jumamosi wiki ijayo ili wapewe elimu ya usalama barabarani ambapo Askari polisi wamesema wapo tayari kufika siku hiyo katika eneo ambalo wataliaandaa ili watoe mafunzo ya sheria za barabarani na haki ya dereva anapotozwa faini
Na Furahisha Nundu
0 comments:
Post a Comment