Home » » MAHAKAMA YA WILAYA MAKETE IMEMPANDISHA KIZIMBANI ASKARI MAGEREZA

MAHAKAMA YA WILAYA MAKETE IMEMPANDISHA KIZIMBANI ASKARI MAGEREZA

Written By kitulofm on Tuesday, 3 December 2013 | Tuesday, December 03, 2013




Juma msam swedi mtumishi wa wizara ya mambo ya ndani kitengo cha askari magereza wilayani Makete amefikishwa katika mahakama ya wilaya kwa kosa la kushawishi na kupokea rushwa iliyokuwa na lengo la kumuachia huru mfungwa anayetumikia kifungo gerezani wilayani hapa.

Akisoma hati ya mashtaka mbele ya hakim mkazi wa wilaya John Kapokoro mwendesha mashtaka wa takukuru mkoani njombe mh Colman Njau amesema kuwa mtuhumiwa anatuhumiwa kwa makosa mawili ambayo aliyafanya mwezi Julai mwaka huu eneola ivalalila wilayani hapa ambapo kosa la kwanza ni kushawish rushwa ya laki mbili na 2.na elifu hasini kutoka kwa Felis Kivengi Sanga ili kuweza  kumuachia huru Godfrey Mahenge ambae bado anaendelea kutumikia kifungo kwa sasa.

Kosa la pili kupokea rushwa kiasi cha laki mmoja kutoka Felic  Mahenge ili kuachia huru mfungwa huyo kinyume cha sheria takukuru sura ya 15kwenye mabano mmoja A ya mwaka 2007.

Hata hivyo mshitakiwa Juma swedi alipoulizwa mahakamani hapo alikana kuhusika na tukio hilo na mh hakimu kapokoro ameiharisha kesi hiyo hadi desemba kumi na tatu mwaka huu na mshitakiwa yupo nje kwa dhamana na upelelezi wa tukio hilo bado unaendelea.



Share this article :

0 comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

KITULO FM LOGO

KITULO FM LOGO
Tusikilize masaa 18 kwa siku kupitia masafa ya 97.0 FM ukiwa wilayani Makete mkoani Njombe na maeneo ya jirani

WASOMAJI WETU

KUMBUKUMBU YA HABARI ZETU

 

Copyright © 2013. KITULOFM BLOG - Haki zote zimehifadhiwa
Imetengenezwa na Edwin Moshi
Inawezeshwa na Kitulo Fm