Home » » MAJONZI:MZEE NELSON MANDELA AFARIKI DUNIA

MAJONZI:MZEE NELSON MANDELA AFARIKI DUNIA

Written By kitulofm on Friday, 6 December 2013 | Friday, December 06, 2013


Mzee Nelson Mandela amefariki dunia kwa mujibu wa CNN mzee Madiba amefariki dunia leo akiwa na umri wa miaka 95.Kwa mujibu wa Rais wa rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma amesema mzee Mandela amefariki Ijumaa usiku baada ya kuugua kwa muda mrefu.Anatarajiwa kuzikwa baada ya siku 10 zijazo


RAIS wa kwanza wa Afrika Kusini na mpinga siasa za ubaguzi wa rangi, Nelson Mandela amefariki nchini humo akiwa na umri wa miaka 95.

Taarifa za kifo chake zimetangazwa na rais wa nchi hiyo, Jacob Zuma ambaye amesema Mandela amefariki majira ya saa 2.50 usiku wa Alhamisi kwa saa za Afrika Kusini.

Mandela amekuwa akisumbuliwa na maradhi kwenye mapafu kwa muda mrefu, alilazwa na baadaye kuruhusiwa kutoka hospitali ambapo mauti yamemkuta akiwa nyumbani kwake mjini Pretoria.

Tayari viongozi mbalimbali duaniani wameshaanza kutuma salamu za rambirambi kwa familia na taifa la Afrika Kusini.

Viongozi hao ni pamoja na Rais Barack Obama wa Marekani na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa (UN), Ban Ki-Moon.
Share this article :

0 comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

KITULO FM LOGO

KITULO FM LOGO
Tusikilize masaa 18 kwa siku kupitia masafa ya 97.0 FM ukiwa wilayani Makete mkoani Njombe na maeneo ya jirani

WASOMAJI WETU

KUMBUKUMBU YA HABARI ZETU

 

Copyright © 2013. KITULOFM BLOG - Haki zote zimehifadhiwa
Imetengenezwa na Edwin Moshi
Inawezeshwa na Kitulo Fm