Home » » MARAIS WAANZA KUWASILI AFRIKA KUSINI

MARAIS WAANZA KUWASILI AFRIKA KUSINI

Written By kitulofm on Monday, 9 December 2013 | Monday, December 09, 2013

Wakuu wa nchi na Serikali 28, wakiwamo 13 wa Afrika, wamethibitisha kushiriki katika matukio yanayohusiana na safari ya mwisho ya Rais wa kwanza wa Afrika Kusini, Nelson Mandela. 
 
                        Nelson Mandela

Serikali ya Afrika Kusini ilisema jana kuwa viongozi 15 waliobaki ni kutoka nje ya Afrika, huku kukiwa na wawakilishi wa mashirika ya kimataifa wakiongozwa na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki – Moon ambaye alitarajiwa kuwasili hapa jana usiku.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Collins Chabane akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari jana alisema Rais wa Marekani Barrack Obama ambaye tayari alishathibitisha kufika, ataambatana na watangulizi wake watatu; George Bush, Jimmy Carter na Bill Clinton pamoja na wake zao.
Chabane alisema Rais wa Brazil ataambatana na watangulizi wake wanne, wakati viongozi wengine mashuhuri na watu maarufu walitarajiwa kuanza kuwasili jana na kwamba baadhi yao watashiriki katika ibada ya kitaifa itakayofanyika katika Uwanja wa Michezo wa FNB, Johannesburg kesho kuanzia saa tano asubuhi.
Kutokana na masuala ya usalama, barabara zote za kuingia katika eneo la Uwanja wa FNB zitafungwa kuanzia saa 12:00 kesho na Serikali imeandaa utaratibu maalumu wausafiri kwa wale ambao watakwenda kuhudhuria tukio hilo.
Hata hivyo, waziri huyo alisema kutokana na ufinyu wa nafasi, baadhi ya watu watakaoshindwa kuingia FNB watapelekwa katika viwanja vingine vya karibu ambako Serikali imeweka televisheni kubwa kwa ajili ya kufuatilia tukio hilo.
Chabane alisema Serikali ya Afrika Kusini imenunua televisheni kubwa zaidi ya 90 ambazo zitafungwa katika kumbi mbalimbali za majimbo nchini kote, ili kuwawezesha wananchi kufuatilia mazishi ya Mandela huko waliko badala ya kurundikana katika maeneo ya matukio.
CHANZO:MWANANCHI

Share this article :

0 comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

KITULO FM LOGO

KITULO FM LOGO
Tusikilize masaa 18 kwa siku kupitia masafa ya 97.0 FM ukiwa wilayani Makete mkoani Njombe na maeneo ya jirani

WASOMAJI WETU

KUMBUKUMBU YA HABARI ZETU

 

Copyright © 2013. KITULOFM BLOG - Haki zote zimehifadhiwa
Imetengenezwa na Edwin Moshi
Inawezeshwa na Kitulo Fm