Home » » SABA WAFA BAADA YA KUFUNIKWA NA MAPOROMOKO YA UDONGO MKOANI KILIMANJARO

SABA WAFA BAADA YA KUFUNIKWA NA MAPOROMOKO YA UDONGO MKOANI KILIMANJARO

Written By kitulofm on Saturday, 14 December 2013 | Saturday, December 14, 2013



Juhudi za kuokoa waliofukiwa zikiendelea


Serikali imeyafunga kwa muda usiojulikana machimbo yote matatu ya moramu na mawe katika kijiji cha Pumwani wilayani moshi baada ya kutokea Maporomoko ya udongo yaliyosababisha vifo vya watu saba hapo jana.

Watu hao wanadaiwa kufukiwa na kifusi wakati wakiwa katika harakati za kuchimba moramu na kupakia kwenye lori lililokuwa limegeshwa kando ya machimbo hayo.



Gari aina ya fuso lenye namba za usajili T 167 AQG ambalo marehemu wa tukio hilo walikuwa wakijaza Moramu likiwa limeangukiwa na ngema iliyokatika na kusababisha vifo vya watu sita.
Maporomoko ya udongo yamekuwa yakitokea mara kwa mara katika miinuko ya mlima Kilimajaro na mara ya mwisho yaligharimu maisha ya watu kumi na moja wilayani Same katika kijiji cha Mamba miamba mnamo mwaka 2007

Safari hii watu saba wameripotiwa kupoteza maisha katika machimbo hayo ambayo ni ajira kwa vijana walio wengi .

Kamanda wa polisi wa mkoa wa Kilimanjaro Bw Robert Boaz amesema, katika ajali hiyo iliyotokea jana jioni watu sita walikufa papo hapo, mwingine amefariki leo asubuhi wakati dereva na utingo wa lori lililokuwa linapakia moramu fuso T 167 AQG wamejeruhiwa na kulazwa hospitali ya rufaa ya KCMC

Kamanda Boaz amewataja waliokufa katika ajali hiyo wakiwemo wanafunzi wawili wa sekondari kuwa ni Marwa Ibrahimu, David Macha, Charles Njiu, Augusti Lyimo, Ludovick Venance Ba Efrem Assey wakati dreva na utingo walionusurika ni Antipuas Babu na Simon Mosha ambao wamelazwa KCMC

Naye kamishna msaidizi wa madini kanda ya kaskazini mhandisi Benjamin Mchwampaka ametaka wakala wa barabara nchini TANROADS mkoani Kilimanjaro Kuchukua hatua za dharura kuimarisha usalama katika machimbo hayo.
Amesema, machimbo hayo yataendelea kufungwa hadi uchunguzi wa ajali hiyo utakapokamilika na kujiridhisha usalama wa wachimbaji.

Kiasi cha vijana 350 watakosa ajira kutokana na katazo hilo la serikali .
Share this article :

0 comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

KITULO FM LOGO

KITULO FM LOGO
Tusikilize masaa 18 kwa siku kupitia masafa ya 97.0 FM ukiwa wilayani Makete mkoani Njombe na maeneo ya jirani

WASOMAJI WETU

KUMBUKUMBU YA HABARI ZETU

 

Copyright © 2013. KITULOFM BLOG - Haki zote zimehifadhiwa
Imetengenezwa na Edwin Moshi
Inawezeshwa na Kitulo Fm