Haya ni madarasa yakiwasubiri wanafunzi januari mwakani
Ndg.Kinana katikati akizungumza,kulia kwake ni Mkuu wa Wilaya ya Makete Mh.Josephine Matiro
Chama cha mapinduzi (CCM) makao Makuu kupitia kwa katibu wake mkuu ndugu Abrahamani Kinana kimeahidi
kutoa mabati 200 kwaajili ya kukamilisha ujenzi wa bweni la kulala wanafunzi
katika shule ya wasichana iliyoko katika kijiji cha Utweve kata ya ukwama wilani hapa
Ndg.Kinana ametoa
ahadi hiyo wakati alipotembalea shule hiyo nakujionea nguvu za wananchi
kwashikiana na viongozi wao kuendelea kujenga majengo ikiwemo bwena la kulala
wanafunzi pia ndugu kinana amempongeza mkuu wa wilaya Maketeb Josophine matiro
kwa kushilikiana vizuri na wananchi na hususani suara la kuchangia ujenzi huo
Aidha mpaka sasa
wananchi waishio kijijini hapo na wale walioko nje ya wilaya kwa kushirikiana na Halmashauri pamoja na TASAF wameweza
kujenga vyumba vitatu vya madarasa,vyoo pamoja na nyumba moja ya kuishi mwalimu ikiwa mpaka sasa wanaendelea na ujenzi wa bweni
litakalo kamilika mapema ili kusaidi wanafunzi hao kuishi shuleni hapo
Shule hiyo inatarajiwa kuanza januari mwakani na
itakuwa ikipokea wanafunzi wa kike kutoka sehemu mbalimbali na ikiwa ni shule
ya kwanza ya wasichana wilayani Makete
Na Riziki Manfred
0 comments:
Post a Comment