Wagonjwa watano wenye maradhi mbalimbali ya moyo wamekwenda nchini India kwa matibabu ambapo wengine watafanyiwa upasuaji.
Wagonjwa hao ambao wanatarajiwa kurejea nchini baada ya wiki nne,
wamefadhiliwa kwa pamoja na Hospitali ya Regency Medical Center, Lions
Club ya Dar es Salaam (Host), Lions club ya Arusha na Prime Bank ya
Kenya.
Shughuli ya kuwaaga wagonjwa hao ilifanyika juzi jioni katika Uwanja wa
Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere ambapo ilihudhuriwa na Rais wa
Lions, Nureen Nathoo, Rais wa zamani wa Lions, Shiraz Rashid,
Mwenyekiti wa kanda wa Lions, Lion Bakary Omary na mratibu wa maradhi ya
moyo katika klabu ya Lions, Dk. Rajni Kanabar.
Kwa mujibu wa Dk. Kanabar, wagonjwa hao watatibiwa katika hospitali ya
CIMS iliyoko mji wa Ahmedabad nchini India kwa punguzo ya gharama ya
Dola 2,500 za Marekani.
“Tunawashukuru wasamaria wema wote waliofanikisha shughuli hii ikiwemo
benki ya Kenya ambayo imetoa dola 5,000 kwenye mradi wa kupeleka
wagonjwa nje,” alisema.
Dk. Kanabar alisema fedha hizo zitatumika katika upasuaji wa mgonjwa
mmoja, tiketi na Dola 200 zitatolewa kwa wagonjwa wote ili ziwasaidie
katika maisha wakiwa ugenini.
Dk. Kanabar alisema tangu kuanzishwa kwa mradi huo, watoto zaidi ya
2,500, vijana na watu wazima wamepelekwa nje kwa ajili ya matibabu ya
moyo.
Gilda Sangwe, ambaye mtoto wake ana tundu kwenye moyo, aliwahsukuru watu
waliojiotolea fedha kwa ajili ya wagonjwa hao kwani bila hivyo
wasingemudu gharama.
Home »
» WATANO WENYE MARADHI YA MOYO KWENDA INDIA KWA MATIBABU
WATANO WENYE MARADHI YA MOYO KWENDA INDIA KWA MATIBABU
Written By kitulofm on Wednesday, 4 December 2013 | Wednesday, December 04, 2013
Related Articles
If you enjoyed this article just click here, or subscribe to receive more great content just like it.
0 comments:
Post a Comment