Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dk. Shukuru Kawambwa, alieleza
hayo bungeni jana alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Meatu, Meshack
Opulukwa (CHADEMA), aliyetaka kujua lini serikali itajenga Chuo cha
Ufundi (VETA) katika Wilaya ya Meatu.
Dk. Kawambwa alisema tayari upembuzi wa stadi zinazohitajika katika ujenzi wa vyuo hivyo umeshafanyika.
“Wilaya ya Meatu ipo katika awamu ya kwanza ambapo mpaka sasa eneo
lenye ekari 50 limetengwa katika kijiji cha Mwambiti kwa ajili ya ujenzi
wa chuo hicho.
“Uongozi wa Wilaya hiyo unatakiwa ukamilishe utaratibu wa kupata hatimiliki ili hatua za ujenzi zifuatwe,” alisema.
Aidha, aliwataka wananchi wa Meatu wakati taratibu za ujenzi wa chuo
hicho zikiendelea watumie vyuo vya ufundi stadi wa jirani.
Alivitaja vyuo hivyo kuwa ni Vyuo vya Ufundi Stadi Mbeya, Tabora na
Mwanza pamoja na Vyuo vya Maendeleo ya Wananchi Kisangwa (Bunda), Mwanva
(Kahama), Malampaka (Maswa), Nzega na Sengerema.
CHANZO:TANZANIA DAIMA
0 comments:
Post a Comment