Akizungumza na kitulo fm kwa
niaba ya mkuu wa polisi wilaya ya makete
OCD ,mkuu wa upelelezi wilaya OC CID
bwana Gozbert komba amesema tukio hilo lilitokea siku ya tarehe tatu
mwezi huu maeneo ya iwawa na wao walipata taarifa siku ya tarehe tano kutoka
kwa bwana Erick Mahenge ambae ni mfanyabiashara wa hapa mjini.
Amesema kuwa walipata taarifa
saa mbili usiku kutoka kwamsamalia mwema Bw.Erick Mahenge kuwa mtoto huyo
alitekwa nyara tarehe tatu januari mwaka majira ya saa saba mchana hadi kukutwa
siku ya tarehe tanosaa saba na nusu mchana ambapo aligundua kutekwa nyara kwa
binti huyo ambaye ni mfanyakazi wake wa kazi za ndani
Hata hivyo amesema kuwa binti
huyo alikutwa akiwaamefungwa kamba katikamiguu yake pamoja na mokono kwa
kutumia kamba ya katani na alikutwa katika nyumba moja akiwa amefungiwa ambayo
haishi mtu (pagalo)
Mara baada ya polisi kupata
taarifa hizo walianza mapema kufuatilia walipomkuta siku hiyo binti alieleza
kwamba anasiku tatu hajaweza kugusa chakula aina yoyote,katika hali hiyo
waliweza kumkamata mtuhumiwa kwani ndiye aliweza kutoa taarifa za mhalifu huyo
Hata hakuna taarifa zozote
zilizokuwa zimetolewakuhusu kubakwa kwake kutoka kwa madaktari ambapo Bw.Komba
amesema kuwa wanasubiri taarifa kutoka wahudumu wa Afya kuhusu uhakika wa
kubwakwa kwa mtoto huyo japokuna dalili zote za kuonesha kubakwa kulingana na
mazingira yanavyoonesha wazi kuwa kuna dalili za kubwakwa kwa mtoto huyo
0 comments:
Post a Comment