Picha na Henrick Idawa
Baadhi ya walimu wakiwa katika picha ya pamoja katika kata ya Lupalilo wilayani hapa
Shule
za msingi kata ya lupalilo wialayani makete zimefanya kikao cha cha walimu wote
wa kata hiyo kwa kuweka malengo na mikakati ya uboreshaji wa taaluma na
mazingira ya shule katika kata ya lupalilo mwaka 2014.kwa lengo la kuinua kiwango
cha elimu katika kata hiyo kutoka aslimia 80% ya matokeo ya darasa la saba
mwaka 2013 hadi wafikie asilimia 85% kwa mwaka huu 2014.Ikiwa watafuata malengo
na mikakati waliojiwekea.
Akisoma
malengo katibu wa elimu kata bw.Orgen Sanga amesema kwa mwaka 2013 walijiwekea
malengo ya kufuta daraja ‘E’ Katika ufaulu wa mitiani wa kuhitimu elimu ya
msingi na kuongeza kuwa mwaka huu 2014 wamejiwekea malengo ya kuhakikisha
kiwango cha ufaulu kutoka asilimia 80% ya sasa mpak 85% ifikapo Disemba
2014,kuongeza ufaulu wa masomo katika madaraja ‘A’,’B’ na ‘C’ na kupunguza
daraja ‘D’ .Pia kuendelea kutopata daraja ‘E’ ambalo wamekwisha lifuta tayari,kuhakikisha
wanafunzi wote wa darasa la pili (2) na tatu (3) wanamudu ABC za elimu ya
msingi,’”KUSOMA’ “KUANDIKA’’ NA ‘’KUHESABU”.(KKK)
BW.SANGA
amesema kufuatia “BRN” wanahakikisha kuboresha michezo na mazingira ya shule na
kuwa na miradi ya shule ili kuongeza kipato cha shule mf.upandaji miti,matunda
kilimo cha pareto na mazao ya chakula,kuwajengea wanafunzi stadi za maisha ili
kuweza wanafunzi kuyakabili mazingira yao na changamoto za maisha.shule zote
kutoa chakula cha mchana na kuandaa mipango ya shule kwa kuzingatia vigezio
vyza BRN Matokeo makubwa sasa na kuwatumia takwimu.
Katika
malengo hao shule hizo zimejiwekea mikakati ya kuwezesha haya yote waliojiwekea
kufikia malengo haya mwaka huu 2014.wamekubaliana kuwa na mikakati ifuatayo
kuongeza muda wa ufundishaji wa kujitolea asubuhi kabla ya vipindi na jioni
baada ya vipindi vya kila siku,kuwa na majaribio ya kila baada kumalizika
mada,majaribioo ya mwezi na mihula kwa madarasa yote,kuwa na mitihani miwili ya
kata kwa darasa la saba na darasa la nne mmoja,kuwepo na kumbukumbu za
kitaaluma kwa kila shule kila shule kuwa na mpango wa jumla wa maendeleo na
kufuatilia utekelezaji wake,kuwepo na mikutano ya wazazi(parents day)mwezi juni
na November mwishoni mwa mwaka na kutoa huduma ya ushauri nasaha na elimu ya
VVU na UKIMWI kwa wanafunzi wakila shule katika kata ya lupalilo
Katika
kikao hicho kilicho anza na kutathimini hali ya ufaulu wa wanafunzi mwaka 2013
kujiunga kidato cha kwanza mwaka 2014,walimu wamelalamikia kutokuwepo kwa
ushirikiano katia ya mzazi,mwanafuinzi na mwalimu katika kuinua elimu,mfumo wa
matumizi ya vitabu ambapo kwa sasa wanatumia zaidi ya aina 5 za vitabu kama
taasisi,oxford,twiga nk.utoro wa wanafunzi kuhudhuria masomo,kuacha kwa masomo
wanafunzi wa kidato cha kwanza na pili kunachangia kushusha hamasa kwa walioko
mashuleni wakisubili kuhitimu.
Walimu
hao wameongeza kuwa upungufu wa walimu ukizingatia idadi kubwa afya zao sio
nzuri hivyo kwa wenye afya kuwa na mzigo mkubwa wa vipindi vya masomo,baadhi ya
watoto kuwa na tatizo la akili hawafundishiki (mtitindio wa ubongo) na
wameshauri kuwepo kwa kitabu kimoja kwa taifa zima ili kuepusha kutofautiana
kwa majibu kati ya shule na shule.
Hata
hivyo mratibu wa elimu kata MEK amesema kwa sasa kuna somo ambalo mwalimu wa
sayansi na maarifa ya jamii wanatakiwa kufundishi ambalo kwa sasa wanasubili
mtaala uletwe kuidhinishwa hivyo walimu wakae wakijua,somo ambalo litahusika na
majanga ya eneo husika na kuwafundisha namna ya kuepuka na kuzuia majanga hayo
mfamo,magonjwa ya mulipuko,mafuriko nk.
Na Henrick Idawa
0 comments:
Post a Comment