Na Martha Magessa
Halmashauri ya manispaa ya Iringa Inatarajia kutoa semina ya huduma ya mfuko wa Afya TIKA kwa viongozi wa dini ifikapo februali 8, 2014.
Mganga mkuu wa Halmashauri ya manispaa ya Iringa Dkt. May Alexander amesema, lengo la kutoa semina ya huduma ya Afya ya Tiba kwa kadi( TIKA) kwa viongozi wa dini ni kuwaamasisha waweze kutoa hamasa kwa waumini wao ili waweze kujiunga katika mfuko huo.
Dkt.Alexander amesema, mfuko wa huduma ya Afya ya TIKA utasaidia kupunguza tatizo la kukosekana kwa dawa katika vituo vya afya na kupata huduma ya matibabu kwa gharama nafuu ya mwaka mzima kwa shilingi 10,000 kwa kichwa.
Ameongeza kuwa, huduma hiyo itaweza kuwasaidia watu wa hali ya chini kupata huduma ya matibabu kwa gharama nafuu ukitofautisha mfuko wa BIMA ya afya wanaokatwa wafanyakazi serikalini kila mwenzi.
Hata hivyo, mganga mkuu huyo wa halmashauri ya manispaa ya Iringa Dkt.Alexander ametoa wito kwa wananchi wa halmashauri hiyo kuchangamkia vitu vyenye manufaa katika maisha yao badala ya kuchangamkia vitu visivyo vya faida kwao.
CHANZO:MJENGWA BLOG
0 comments:
Post a Comment