Home » » JESHI LA POLISI IRINGA LATOA TAMKO KWA YEYOTE ATAKAYEONEKANA KUVURUGA AMANI

JESHI LA POLISI IRINGA LATOA TAMKO KWA YEYOTE ATAKAYEONEKANA KUVURUGA AMANI

Written By kitulofm on Tuesday, 25 February 2014 | Tuesday, February 25, 2014

Yonna Mgaya
IRINGA
Jeshi la polisi mkoani Iringa limesema kuwa halipo tayari kuvumilia vitendo au mtu na mfuasi wa chama chochote atakaeonesha kutaka  kuvuruga amani  katika kampeni za chaguzi jimbo la kalenga.
Akizungumza na waandishi wa habari kaimu kamanda wa polisi mkoani hapo Peter Mkakamba amesema kuwa mtu yeyote na mfuasi wa chama atakaeonesha dalili za kuvuruga amani iliopo katika jimbo la kalenga atawajibishwa kutokana na sheria na taratibu,ambapo uzoefu unaonyesha kuwa katika chaguzi ndogo za madiwani zilizo pita  katika kata za Nduli,Ibumu na Ukumbi mkoani hapo kuligubikwa na  vitendo vilivyoashiria uvunjifu wa amani.
Kaimu kamanda ameongeza  kuwa katika chaguzi hizo za udiwani ambazo ziligubikwa na vilivyodhaniwa kuwa na uvunjifu wa amani mfano wafuasi wa vyama kushambuliana,kujihami kwa kutembea na marungu, mapanga kwaajili ya kuwakabili wapinzani wao hasa pale walipotengeneza mfumo wa  kampeni za nyumba kwa nyumba jambo ambalo si sahihi.
Aidha amesema sababu zinazofanya uvunjifu wa amani ni pamoja na kuingiliana kwa ratiba za kampeni na viwanja na wakati mwingine kujichukulia sheria mkononi kwa kuwapiga watu  kwa kuhisia kuwa ni wapinzani wa vyama vyao.
Hata huvyo Mkakamba amesisitiza kuwa jeshi la polisi limejipanga kiukamilifu ili kuakikisha shughuli za kampeni na na uchaguzi zinafanya katika hali ya amani na utulivu.
Share this article :

0 comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

KITULO FM LOGO

KITULO FM LOGO
Tusikilize masaa 18 kwa siku kupitia masafa ya 97.0 FM ukiwa wilayani Makete mkoani Njombe na maeneo ya jirani

WASOMAJI WETU

KUMBUKUMBU YA HABARI ZETU

 

Copyright © 2013. KITULOFM BLOG - Haki zote zimehifadhiwa
Imetengenezwa na Edwin Moshi
Inawezeshwa na Kitulo Fm